NA WAMJW-IRINGA
SERIKALI
kupitia Wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
imerahisisha ukusanyaji wa takwimu za vifo vinavyotokea kwenye ngazi ya
jamii nchini kwa kugawa vifaa maalumu vya kukusanyia takwimu hizo kwa
Maafisa afya katika kata za mkoa wa Iringa.
Hayo
yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya
jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya
wakati akikabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa
kukusanyia takwimu hizo kwa Maafisa Afya leo Mkoani Iringa.
“Takwimu
zitakazokusanywa kuhusu vifo na Maafisa hawa wa afya kutokana na
Mifumo hii zitawasaidia madaktari kujadili changamoto pamoja na sababu
za vifo hivyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo na kuweza kupunguza
idadi ya vifo nchini” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha,Dkt.
Mpoki Ulisubisya amesema kuwa takwimu hizo zikikusanywa kikamilifu
zitasaidia kutoa elimu kwa jamii na kupunguza imani za kishirikina kwa
wananchi kwani zitaleta picha sahihi ya kugundua vyanzo vya vifo hivyo
kwenye jamii husika.
Hata
hivyo Dkt. Ulisubisya amewataka maafisa hao kutumia vifaa hivyo kwa
matumizi ya kazi ya kukusanyia takwimu na sio matumizi binafsi na kama
itatokea afisa afya yeyote atakayehama kituo cha kazi basi arudishe
ofisini kwa ajili ya mtumishi mwingine atakayekuja.
Kawa
upande wake Kaimu katibu Tawala wa Mkoa iringa Bw. Fikira Kissimba
amesema kuwa mfumo huo wa ukusanyaji taarifa zitasaidia pia
uandikishwaji wa mirathi ya marehemu wakati ndugu husika anapokwenda
kufungua mirathi yake mahakamani.
Naye
Mratibu wa usajili wa Takwimu wa Masula muhimu ya Binadamu nchini Dkt.
Gregory Kabadi amesema kuwa jumla ya Kompyuta kibao (Tablets)
zilizogawiwa ni 106 kwa kila kata ya mkoani Iringa na thamani yake ni
takribani shilingi Milioni 61.5.
Aidha
, Dkt Kabadi amesema kuwa zoezi hilo limeanza kwa majaribio katika
halmashauri tano kwenye mikoa mitatu ikiwemo Pwani,Tanga na Morogoro na
kufanya tathimini ya utekelezaji wa mifumo hiyo katika mkoa wa Iringa
kabla ya kutumika nchi nzima.
Kwa upande wake Afisa afya wa
kata ya Kitwilu Bw. Wilson Ntagondwa amesema kuwa kupitia mfumo huo
waliokabidhiwa itawasaidia kukusanya takwimu kwa urahisi hivyo kupelekea
kujua sababu zinazosababisha vifo na kusaidia kupanga maendeleo
No comments :
Post a Comment