Baadhi ya mabaki ya Mjusi mkubwa
mwenye urefu wa mita 13.7 kwenda juu aliyegunduliwa miaka 100 iliyopita
katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi aliyepo katika makumbusho nchini
Ujerumani ambao kwa sasa Serikali ya Tanzania imeanza mazungumzo kuona
jinsi gani itaanza kupata gawio lake kupitia watalii.
…………………………………………………..
Serikali ya Tanzania kupitia
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga imesema ipo
kwenye hatua za awali za mazungumzo na Serikali ya Ujerumani kuona jinsi
itakavyofaidika na mapato yatokanayo na utalii kupitia mabaki ya Mjusi
mkubwa ‘’Dinosaurs ambaye ni kivutio cha kikubwa cha utalii katika
jumba la Makumbusho nchini Ujerumani
Mjusi huyo kwa jina la kitaalamu
anaitwa Dinosaur ambapo mabaki yake yalivumbuliwa miaka 100 iliyopita
katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi, yalikusanywa na kupelekwa
nchini Ujerumani ambako wataalamu waliyaunda na kisha kuyaweka kwenye
Makumbusho hiyo.
Amesema lengo la mazungumzo hayo
ni kutaka kujua kiasi gani cha mapato yanayokusanywa na namna gani
wanavyoweza kugawana mapato hayo yatokanayo na watalii kupitia mjusi
huyo baina ya Serikali hizo mbili.
Amesema mwelekeo wa mazungumzo
hayo yaitapelekea Serikali ya Tanzania kufanya uamuzi wa kumrudisha
mjusi huyo au kumuacha kule kule lakini akiwa analiingizia pato
taifa
Ameyabainisha hayo jijini Dar es
Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na mIkakati
ya Serikali ya kuendeleza vivutio vya utalii kwa mikoa ya Kusini.
Hata hivyo, Mhe.Hasunga amesema
uamuzi wa kumrudisha mjusi huyo nchini utakuwa mgumu kwa vile sehemu
kubwa ya mjusi huyo ameunganishwa unganishwa kwa kutumia vifaa maalumu.
Ameongeza kuwa kutokana na jinsi
alivyounganishwa unganishwa na anakadiri wa kuwa na urefu wa mita 13.7
kwenda juu hivyo kumsafirisha itakuwa ngumu.
Katika hatau nyingine, Mhe
Hasunga amesema hadi hivi sasa Serikali ya Ujerumani haijaweza kuweka
bayana kiasi cha mapato yanayokusanywa kupitia Mjusi huyo licha ya kuwa
Serikali hiyo imekuwa ikifadhili miradi mingi ya uhifadhi nchini.
“Tunaamini kuwa pesa
wanazofadhili miradi mingi ya Uhifadhi imekuwa inatokana na makusany
okupitia Mjusi huyo Mkubwa” amesema Hasunga
Hata hivyo,kuendelea kuwepo kwa
masalia ya mjusi huyo katika Makumbusho hiyo kuna manufaa makubwa kwa
vile anatambuliwa kuwa ni wa kutoka Tanzania,Hivyo ni Balozi wa Utalii
na utafiti wa kisayansi anayeitangaza Tanzania sehemu mbalimbali
duniani.
No comments :
Post a Comment