Kaimu Mkurugenzi wa idara ya
Gharama za Uchaguzi na Misaada Bi. Piencia Kiure akifungua mafunzo ya
siku mbili juu ya Sheria za Gharama za Uchaguzi na Maadili ya Vyama vya
Siasa yanayoendelea leo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili
wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe.
Jaji Francis Mutungi (wa tatu kushoto) akisisitiza jambo wakati wa
majadiliano katika mafunzo ya siku mbili juu ya Sheria za Gharama za
Uchaguzi na Maadili ya Vyama vya Siasa yaliyoanza leo katika ukumbi wa
mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam.
Bi. Esther Mwanri, Mratibu wa
mafunzo akitoa mada kuhusu maana, lengo la Sheria ya Gharama za Uchaguzi
na jinsi ya ujazazi wa fomu za Gharama za Uchaguzi.
Mmoja wa washiriki akichangia hoja wakati wa majadiliano
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini wakati wa mafunzo
Msajili wa Vyama vya Siasa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo
………………………
Maafisa wa Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa wanaojiandaa kushiriki katika uangalizi wa kampeni za
uchaguzi unaotegemea kufanyika Decemba 2 mwaka huu, wameaswa kutekeleza
majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ili kujikita katika kuhudumia Vyama
vyote kwa usawa.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Gharama za Uchaguzi na Misaada Bi. Piencia Kiure
wakati akifungua mafunzo ya siku mbili juu ya Sheria za Gharama za
Uchaguzi na Maadili ya Vyama vya Siasa kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya
Siasa Mhe. Jaji Francis S. K Mutungi yanayoendelea kufanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es
Salaam.
Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo,
mratibu wa mafunzo, Bi. Esther Mwanri amesema kuwa mafunzo hayo ni
muendelezo wa mafunzo ambayo hutolewa na ofisi hiyo kwa maafisa ambao
hushiriki katika uangalizi wa chaguzi za Madiwani, Wabunge na Urais
yakiwa na lengo la kuwakumbusha washiriki taratibu na sheria mbalimbali
zinzzozimamiwa na Ofisi ya msajili wa Vyama vya Siasa na zinazotakiwa
kutekelezwa na wagombea na vyama vya siasa nyakati za chaguzi.
Bi. Mwanri amebainisha kuwa baadhi
ya mada ambazo zimewasilishwa na zitakazowasilishwa ni pamoja na maana
na lengo la Sheria ya Gharama za Uchaguzi, matendo yaliyokatazwa katika
kampeni za uchaguzi, Fomu zinazohitajika kujazwa na wagombea na vyama
vya siasa na namna ya kuzijaza. Elimu ya maadili ya vyama vya siasa,
haki ya vyama vya siasa, wajibu wa Vyama vya Siasa na wajibu wa Msajili
wa Vyama vya Siasa.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa ni taasisi iliyopo kwa mujibu wa kisheria ambayo ina wajibu wa
kusimamia vyama vya siasa nchini ili viweze kutekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi.
No comments :
Post a Comment