Wednesday, October 31, 2018

Madeni ya pensheni waliokuwa PSPF yaanza kulipwa

MMGL0274.jpg

Meneja Kiongozi Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa PSSSF, Eunice Chiume. Picha na maktaba yetu;

Na Christian Gaya. majira Jumatano, 31 Agosti 2018, www.majira.co.tz
IKUMBUKWE ya kuwa katika mkakati wa kuboresha huduma na kupunguza matumizi katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini, Serikali iliamua kuunganisha  Mifuko minne ya PSPF, PPF, GEPF  na LAPF na kuunda Mfuko mmoja unaojulikana kama Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Hivyo basi, baada ya kutangazwa kuanza kwa Mfuko wa PSSSF, pamoja na mambo mengine uongozi mpya ulikuwa na jukumu la kwanza la kulipa madeni ya malipo ya mkupuo kwa wanachama wa waliokuwa wa mfuko wa pensheni wa PSPF.

Kulingana na kiongozi mkuu wa idara ya masoko na uhusiano wa PSSSF Eunice Chiume anasema idadi yao ilikuwa ni wastaafu wapatao 7,924 wenye jumla ya Sh. bilioni 738.43. “mpango huu wa kulipa madeni haya uliidhinishwa na Bodi ya PSSSF kwa kuzingatia mtiririko wa kifedha kwa kipindi cha miezi 6 kuanzia Agosti 2018” alisema Chiume.
Alisema kwa Agosti 2018 tu Mfuko wa PSSF uliwalipa wastaafu  wapatao 896 wa Julai 2017, ambapo kati hao 755 wakiwa wa fao la kustaafu na wapatao 141 wakiwa wanufaika wa fao la urithi na hivyo basi Mfuko ulitumia jumla ya Sh.65,381,743,855.48 kwa wastaafu wote;
“Orodha iliyohakikiwa na Hazina na kupitishwa kwa ajili ya malipo ina wastaafu wa umri wapatao 5,904. Kati ya hao hundi zipatazo 1,123 zenye jumla ya Sh. 94,484,375,322.57 zikiwa ni zile zilizotakiwa kulipwa kati ya mwezi Agosti mpaka Novemba 2017 zilitolewa kwa malipo kati ya Oktoba 5 na Oktoba mwaka huu.   
Ambapo kati ya Wastaafu wapatao 814 wa mwezi Desemba 2017 wanategemewa kulipwa mwishoni mwezi huu wa Oktoba 2018,” Chiume alifafanua.
Wakati kwa Novemba 2018 watalipwa wastaafu 1,603 wa mwezi Januari – Machi 2018. Kwa Disemba 2018 watalipwa wastaafu 931, wakati wa Aprili - Mei 2018 na waliobaki 1,372 watalipwa Januari 2019.
Alisema wastaafu wapatao 1,292, Hazina ilishauri wafanyiwe uhakiki zaidi kabla ya kuanza kulipwa pensheni zao, ambapo kati yao wapo waliondoka kazini kwa kufukuzwa, kuacha kazi, kuwa na umri zaidi ya miaka 60, vyeti feki na marekebisho ya muundo.
Malipo ya wastaafu walioingia kwenye Mfuko mpya wa PSSSF kuanzia tarehe mosi Agosti 2018 na kuendelea, wao wanaendelea kulipwa, ambapo hadi sasa madai yapatayo 326 yameshalipwa. “Lengo Letu ni kuendelea kuwalipa ndani ya muda unaotajwa kisheria hadi madai ya nyuma yatakapokamilika na baada ya hapo watalipwa mapema zaidi.” Alifafanua zaidi.
Alisema wakati madai ya kipindi kabla ya kuanza kwa Mfuko wa PSSSF ambayo hayakuwa yamelipwa na mifuko kutokana na sababu mbalimbali yameletwa makao makuu kwa ajili ya kukamilishwa na kuandaliwa malipo.  Madai hayo ni jumla ya 3,876 yakijumuisha madai ya mafao ya uzazi, malipo ya mfumo wa hiari, kujitoa na kupunguzwa kazi. “Madai hayo sasa yameletwa hapa PSSSF makao makuu Dodoma kwa uchambuzi na malipo kwa madai yanayostahili,” Eunice alieleza.



No comments :

Post a Comment