Naibu
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony P. Mavunde leo Oktoba 31, 2018 amekabidhi kwa Vijana
wakulima na SIDO awamu ya kwanza ya ruzuku ya jumla ya Tsh 1,200,000,000
iliyotolewa na USAID katika utekekelezaji wa mradi wa “Feed the Future”
unaotarajia kuwafikia Vijana 33,000 katika mikoa ya Iringa,Mbeya na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Makabidhiano
hayo yamefanyika leo katika Kata ya Kiwele,Kalenga Mkoani Iringa ambapo Mh
Mavunde amechukua fursa hiyo kuwashukuru USAID kwa namna wanavyosaidiana na
serikali kutatua changamoto zinazoakabili vijana na kutumia fursa kuwataka
Vijana nchi nzima kushiriki kwenye sekta ya Kilimo na kuahidi kwamba serikali
itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kilimo ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika.
Wakuu
wa Wilaya za Kilolo na Mbeya,kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Iringa na Mbeya,*Mh
Asia Abdallah* na Mh Paul Ntinika wameahidi kutoa ushirikiano katika
utekelezaji wa program hii na kuhakikisha kwamba malengo ya program hii
yanafikiwa na vijana wengi zaidi kunufaika.
Akitoa
maelezo ya awali Mkurugenzi wa Uchumi wa USAID Bi Terhi Majanen ameeleza kwamba
ruzuku hiyo ya awamu ya kwanza inalenga kwenda kuzalisha ajira 735 na
uanzishwaji wa viwanda vidogo 200.
No comments :
Post a Comment