Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akifurahia jambo wakati alipokutana na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dk. Maulid Banyani wa
kwanza kulia, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC Dk Sophia Kongela wa
pili kulia walipokuenda kujitambulisha ofisini kwake Dodoma, wengine kushoto ni
Naibu Waziri wa Ardhi Dk Angeline Mabula na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Doroth
Mwanyika.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dk. Angeline Mabula akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHC
Dk Sophia Kongela kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kushika nafasi hiyo, alipotembelea ofisi
za Wizara ya Ardhi jijini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi na Naibu wake Dk Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja
na uongozi mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya NHC Dk. Sophia Kongela wa pili kulia na Mkurugenzi Mkuu Dk.
Maulid Banyani.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi akimkabidhi ripoti Mapitio ya Muundo wa Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC Dk Sphia Kongela leo
jijini Dodoma.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa maelekezo kwa
Mkurugenzi wa Mipango Miji Wizara ya Ardhi Profesa John Lupala wakati
akioneshwa ramani ya mji wa Serikali uliopo Dodoma.
No comments :
Post a Comment