Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto( Idara kuu ya Maendeleo ya
jamii) Dkt. John Jingu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu nyongeza ya siku 14 zaidi zilizotolewa kwa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi
na za fedha za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla ya
kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Baadhi ya Wakuu wa Idara na
Vitengo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) wakifuatilia tamko la Katibu
Mkuu Dkt. John Jingu la kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika ya Yasiyo
ya Kiserikali kuhakikisha yanawasilisha taarifa za miradi na za fedha
zilizokaguliwa za mwaka 2016 na 2017 kwa Msajili wa Mashirika hayo kabla
ya kufutiwa usajili wao. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
Katibu Mkuu wa Braza la NGOs
nchini Bw. Ismail A. Suleiman akieleza kuridhishwa kwake na kanuni mpya
za NGOs (2018) ambazo zimezingatia matakwa ya kanuni za maadili katika
kuboresha utendaji wa NGOs wakati wa kikao cha Idara kuu ya Maendeleo ya
Jamii kilichoeleza kuongeza siku 14 zaidi kwa Mashirika hayo
kuwasilisha taarifa za miradi na fedha kwa Msajili wa NGOs. Picha na
Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
…………………..
Na Mwandishi Wetu Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa siku kumi nne zaidi
(14) kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuhakikisha yanawasilisha
taarifa za miradi na za fedha za mwaka 2016 na 2017 zilizokaguliwa kwa
Msajili wa Mashirika hayo kabla ya kufutiwa usajili wao.
Tamko hilo limetolewa leo jijini
Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo
la Serikali lililotolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Ufafanuzi ulitolewa kuwa,
“Siku ya tarehe 28 Septemba, 2018, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alikutana na
wawakilishi wa vyombo vya habari na kutoa maagizo yakuyataka Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali kuwasilisha taalifa zao kwa Mashirika hayo ikiwa ni
pamoja na taarifa za miradi na taarifa za fedha zilizo kaguliwa kwa
mwaka 2017 na 2018”, alibainisha DKT. Jingu.
Dkt Jingu amefafanua kuwa,
maagizo hayo yalipaswa kutekelezwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia
tarehe 28.9.2018 ya agizo lilipotolewa na Serikali. Hata hivyo
imeelezwa kuwa mwitikio wa utekelezaji umekuwa wa kuridhisha kutokana na
ukweli kuwa Mashirika mengi yamezingatia maelekezo ya Serikali.
Aidha, Wizara imepokea maombi
kutoka Ofisi ya Baraza la Taifa la NGOs na baadhi ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali wakiomba kuongezwa muda kidogo ili waweze kukamilisha
maandalizi ya taarifa zao na kuziwasilisha haraka. Kutokana na kutambua
nafasi ya NGOs katika maendeleo ya Taifa, Serikali imeridhia kuongeza
siku kumi na nne (14) kuanzia leo (31/10/2018) ili kuwapa fursa wale
ambao walikuwa bado hawajatimiza maelekezo hayo kutokana na sababu
mbalimbali kufanya hivyo. “Nasisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine
wa nyongeza kwa wale ambao hawatakuwa wamewasilisha taarifa hizo ndani
ya muda wa nyongeza. Shirika ambalo litakuwa halijawasilisha taarifa
Wizara itachukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria”. alisisitiza Dkt.
Jingu.
Katibu Mkuu huyo amerudia
kuhakikishia umma kuwa, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa NGOs
kwa maendeleo ya nchi. Msisitizo wa Serikali wa uwazi na uwajibikaji
unalenga kuwezesha Serikali, wananchi na wadau wa maendeleo kutambua
vizuri zaidi mchango wa NGOs katika shughuli za maendeleo. Pia kama
ilivyo kwenye sekta nyingine, uwazi na uwajibikaji utasaidia kuzuia
matumizi mabaya ya rasilimali zinazotolewa na wadau wa maendeleo kupitia
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuwa kichocheo katika kufikia azma
ya maendeleo jumuishi.
Akizungumza katika Mkutano
huo, katibu Mkuu wa Braza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Ismail
A. Suleiman ameishukuru Serikali kwa kuridhia ombi nyenyekevu la
kuongeza muda wa kuwasilisha taarifa za fedha na miradi ili kuwezesha
NGOs kutimiza takwa la agizo hio.
Bw. Ismail amebainisha kuwa
kanuni mpya za NGOs (2018) zilizotangazwa tarehe 19/10/2018 kwa kiasi
kikubwa zimezingatia utekelezaji wa kanunni za maadili; hivyo Braza la
NGOs litaunda kikosi kazi kuzipitia na kutoa maoni kwa lengo la
kuboresha utendaji wa NGOs kwa mujibu wa matakwa ya kisheria, kanuni na
taratibu.
Baraza la NGOs limewataka
wanachama wake wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuhakikisha kuwa
wanatekeleza kazi zao kwa mujibu wa katiba za mashirka yao ili
kushirikiana na Serikali katika kuchochea ustawi na maendeleo ya watu
hususan kunufaisha makundi yote ya kijamii.
Maagizo haya kwa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali yanakuja mwezi mmoja baada ya AGIZO LA Serikali
kutolewa likizitaka NGOs zote nchini pamoja na mambo mengine kuwasilisha
taarifa zao za kazi na matumizi ya fedha ya miradi wanayoitekeleza.
Imeelezwa kuwa hadi taarifa hii inatolewa zaidi ya Mashirika 2000
yamewasilisha taarifa zao na wengi wanaendelea kuitiki maelekezo hayo.
No comments :
Post a Comment