Naibu waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Tate William Ole-Nasha
akitoa Taarifa ya Wizara ya Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Mkakati
wa Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka mbele ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria leo katika Ofisi za Bunge
Jijini Dodoma. Mheshimiwa Ole-Nasha alimwakilisha Waziri wa Katriba na
Sheria Prof. Paramagamba Kabudi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Najima Giga akifurahi
jambo wakati kamati hiyo ilipokutana na Wizara ya Katiba na Sheria
kupokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Wizara hiyo kuhusu Mkakati wa
Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Kushoto kwa
Mheshimiwa Giga ni katibu wa Kamati hiyo Ndg. Kagisa.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Naibu
waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa
Tate William Ole-Nasha akitoa Taarifa ya Wizara ya Wizara ya Katiba na
Sheria kuhusu Mkakati wa Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Taifa ya
Mashtaka leo katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE.)
No comments :
Post a Comment