Wednesday, October 31, 2018

BREAKING NEWS: MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ AFIKISHWA KORTINI AKIKABILIWA NA MASHITAKA 75 LIKIWEMO LA UTAKATISHAJI FEDHA


1

MDOGO wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, anayetambulika kwa jina la Akram Aziz leo Oktoba 31, 2018 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka 75, yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na silaha za aina mbalimbali pamoja na kutakatisha fedha zaidi ya Dola za Marekani 6494.

2 3

MDOGO wake mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, anayetambulika kwa jina la Akram Aziz leo Oktoba 31, 2018 akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka 75, yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na silaha za aina mbalimbali pamoja na kutakatisha fedha zaidi ya Dola za Marekani 6494.
……………………
*Yamo ya kutakatisha fedha, kukutwa na nyara za Serikali

Na  Karama Kenyuko,Globu ya jamii


MDOGO wake mfanyabishara maarufu nchini Rostam Aziz, anayetambulika kwa jina la Akram Azizi leo Oktoba 31, 2018 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka 75 yakiwemo ya mashtaka 71 ya kukutwa na silaha za aina mbali mbali pamoja na kutakatisha fedha za Marekani dola 9018.
Mshtakiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 82/2018 pia anakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya Sh. milioni 108, risasi 6496 pamoja na kosa la kukutwa na nyama ya Nyati kilogramu 65 yenye thamani ya Sh.milioni 4.35 bila kuwa na kibali.


Ambapo anadiwa kulitenda kosa hilo Oktoba 30,2018  katika eneo la Oysterbay Kinondoni Dar es Salaam.


Mshtakiwa amesomewa mashtaka yake na jopo la mawakili wawili wa Serikali likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi aliyekuwa akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Augustine Rwizile.


Akisoma hati ya mashtaka hayo leo mahakamani hapo Wakili Kadushi amedai katika shtaka la utakatishaji mshtakiwa anadaiwa kati ya Juni 2018 na Oktoba 30, 2018 katika eneo la Oyesterbay, mtuhumiwa alijipatia jumla ya dola za Marekani 9018 huku akijua  fedha ni zao la kosa tangulizi la kujihusisha na biashara haramu ya nyara za Serikali pamoja na kukutwa na silaha bila kibali.
Katika mashtaka ya kukutwa na risasi, mshtakiwa anadaiwa kuwa Oktoba 30 mwaka 2018 (Jana) huko Oyesterbay, alikutwa na risasi 4092 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa kibali cha silaha.
Pia imedaiwa Oktoba 31, 2018 (leo) huko huko Oyesterbay mshtakiwa alikutwa na risasi 2404 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa silaha.
Baada ya kusomewa makosa hayo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama hiyo  haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.


Kwa mujibu wa upande wa mshtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo mshtakiwa amerudishwa rumande.Kesi imeahirishwa hadi November 11,2018.

No comments :

Post a Comment