Meneja wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Masawa Masatu akizungumza wakati wa semina
ya wafanyabiashara iliyofanyika jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu
ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi,
Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo
takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Tanga Monica Kinara akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara
iliyofanyika jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na
Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi
ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150
wamehudhuria semina hiyo.
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi
Diana Masalla kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu
akiwasilisha mada kuhusu Mabadiliko ya Sheria za Kodi wakati wa semina
ya wafanyabiashara iliyofanyika jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu
ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi,
Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo
takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
Afisa Maadili Mwandamizi Adelaida
Rweikiza kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu
akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili wa Watumishi wa TRA wakati wa
semina ya wafanyabiashara iliyofanyika jijini Tanga kwa lengo la kutoa
elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi,
Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo
takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
Baadhi ya wafanyabiashara
waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya
Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka
2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria
semina hiyo. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
Na Veronica Kazimoto
Tanga
19 Septemba, 2018
Wafanyabiashara
wapatao 150 mkoani Tanga wameelimishwa kuhusu Msamaha wa Riba na
Adhabu
ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka
2018 na Mfumo wa Maadili wa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara hao kujua kwa undani
masuala yanayohusu kodi pamoja na kuwahi kuomba msamaha wa riba na
adhabu ambapo mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Novemba, 2018.
Akifungua
semina ya wafanyabiashara hao mkoani hapa iliyoandaliwa na TRA, Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa Monica Kinara amesema kuwa, elimu hiyo imekuja
wakati muafaka na siyo tu itawasaidia kujua masuala ya kodi bali wale
wenye malimbikizo ya madeni ya kodi watanufaika na msamaha huo na
hatimaye wataweza kulipa kodi kwa wakati.
“Ninawashukuru
sana TRA kwa kuleta elimu hii hapa mkoani kwetu na ni matumaini yangu
kuwa, wafanyabiashara mtatumia fursa hii vizuri ili iwasaidie kuelewa
masuala mbalimbali yanayohusu kodi na hasa msamaha wa riba na adhabu ya
kodi ili muweze kuomba msamaha huo ndani ya muda uliopangwa,” alisema
Kinara.
Naye,
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla
amewaeleza wafanyabiashara hao kwamba, ni jukumu la kila mwenye
malimbikizo ya madeni ya kodi kuwahi kuomba msamaha wa riba na adhabu
akiwa ameambatisha dodoso maalum la msamaha huo pamoja na ritani ya
taarifa za Mlipakodi.
“Huu
ni msamaha maalumu hivyo ni muhimu mzingatie kutuma maombi kabla ya
tarehe 30 Novemba mwaka huu, kinyume na hapa mtaikosa fursa hii muhimu
ambayo ina lengo la kuwapunguzia mzigo wa kodi,” alisisitiza Masalla.
Kwa
upande wake Mfanyabiashara wa Nyumba za Kulala Wageni Teti Mathias
ameshukuru ujio wa elimu hii mkoani Tanga na kuiomba TRA iwe na
utamaduni wa kutoa elimu hizi katika ngazi ya Kata na Tarafa ili
wafanyabiashara wengi waweze kupata uelewa wa kutosha kuhusu masuala
mbalimbali ya kodi.
Msamaha
maalum wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya kodi unatolewa
kwa asilimia 100 kwa wafanyabiashara wenye malimbikizo hayo ambao
watakidhi vigezo vilivyowekwa katika utaratibu wa kuomba msamaha huo.
No comments :
Post a Comment