Wednesday, September 19, 2018

NMB YATOA HUNDI YA MILIONI 100 KWA AJILI YA MKUTANO MKUU WA ALAT


DSC_0437
Kaimu Katibu Mkuu wa ALAT Bw.Abadallah Ngodu akizungumza na Viongozi  pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo Pichani) wakati wa kutoa Taarifa ya Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 24 hadi 28 Jijini Dodoma
DSC_0444
Mwenyekiti wa ALAT Taifa Bw.Gulamhafeez Mukadamu akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano Mkuu wa ALAT Unaotarajiwa kufanyika Septemba 24 hadi 28 mwaka huu jijini Dodoma.
DSC_0457
Bw. Nsolo Mlozi Meneja wa NMB kanda ya Kati akizungumza na Waandishi wa habari baada ya Benki yao kutoa Ufadhili wa Mkutano Mkuu wa ALAT Unaotarajia kufanyika Septemba 24 hadi 28 Jijini Dodoma
DSC_0460
Bw.Nsolo Mlozi Meneja NMB Kanda ya kati akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhafeez Mukadamu, fedha hizo ni kwa ajili ya kufanikisha mkutano huo Unaotarajia kufanyika Septemba 24 hadi 28 jijini Dodoma
……………………………
Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma
 Jumuiya  ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) intarajia kufanya mkutano wake mkuu wa 35 Septemba 24 hadi 28 mwaka huu Jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais
Dkt.John Pombe Magufuli.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mwenyekiti wa ALAT Taifa Gulamhafeez Mukadamu,amesema kuwa maandalizi ya Mkutano huu yameshakamilika na utafanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Hapa na kuonngeza kuwa Jumuiya ya Tawala ya Mitaa Tanzania ni chombo wakilishi na sauti ya pamoja ya Mamlaka ya serikali za mitaa inayounganisha halmashauri zote za majiji,Manispaa,Miji na wilaya Tanzania bara.
Na pia ameeleza kuwa Jumuiya jiyo Ilianzishwa mwaka 1984,Desemba 13 Mjini Dodoma baada ya kureshwa kwa mfumo wa Serikali za Mitaa kwa Sheria Sura Na.288 ya Sheria ya nchini.
“Majukumu ya msingi ya Jumuiya kwa mujibu wa katiba ni kuwakilisha haki maslahi ya serikali za mitaa katika vyombo mbalimbali nchini na nje ya nchi, kushawishi mabadiliko ya sera na sheria kwa lengo la kuwezesha utekelezaji mzuri wa dhana ya kupeleka madaraka kwa wananchi”amesma Mukadamu
Aidha amesema kuwa Alat hutoa huduma za kusaidia Mamlaka ya Serikali za Mita katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuboresha ufanisi na Utekelezaji wa majukumu yao na kuwa jukwaa la upashanaji wa habari na kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Jambo lingine ni kujadili taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa shughuli za Jumuiya,kupokea na kujadili taarifa ya fedha ya jumuiya na kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi jumuiya kwa mwaka 2018 na 19.
Mkutano Mkuu wa Alat unatarajiwa kuhudhuliwa na wenyekiti wa Halmashauri zote,Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wabunge mmoja kutoka kila Mkoa wa Tanzania bara na kufanya idadi ya washiriki kuwa zaidi ya 500 na kutakuwa na waalikwa kutoka nchi mbalimbali.
Hata hivyo ALAT imetoa wito kwa mashirika na wadau mbalimbali kufadhili mkutano huo ikiwa ni pamoja na sehemu ya kutangaza bidhaa zao kwa lengo la kufanikisha mkutano huo kwa manufaa ya kuboresha Maisha ya watanzania.
Katika Kufanikisha Mkutano huo Benki ya NMB imekabidhi Hundi ya shilingi Milioni 100 kama sehemu ya faida inayopatikana kutoka benki hiyo nchi.
Bw.Nsolo Mlozi ambaye ni Meneja NMB Kanda ya kati akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gulamhafeez Mukadamu,Mlozi alisema fedha hiyo ni kwa ajili ya kufanikisha mkutano huo wa ALAT.
Mlozi amaesema kuwa NMB inatambua mchango mkubwa ambazo hutolewa na halmashauri katika kufanikisha shughuli za maendeleo na katika harakati za kuhakikisha halmashauri zinafanikisha katika ukusanyaji wa mapato NMB kwa sasa imeweza kuunganisha halmashauri 160 katika mfumo wa Elekroniki kwa ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine za Elekroniki.
Katika Mkutano Mkuu wa ALAT Wadau pamoja na Viongozi wa Serikali wanatarajia kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni kuona ni namna gani ya  kuishauri Serikali juu ya urudishwaji wa vyanzo vya mapato vilivyochukuliwa na Serikali Kuu na kuzifanya halmashauri kuwa na hali mbaya ya kiuchumi.
Aidha halimashauri nyingi  zimekuwa na uchumi kiduchu unatokana na serikali kuchukua vyanzo vingi vya mapata na kuviingiza katika serikali kuu jambo ambalo lilioneonekana kuwa kikwazo cha maendeleo katika halimashauri nyingi kwa kushindwa kuwa na vyanzo vya mapato vya kutosha kama ilivyokuwa hapo awali.

No comments :

Post a Comment