Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza na wanachama wa Skimu ya
Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, wakati wa yeye na timu yake
walipofanya ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya
umwagiliaji unaotekelezwa na skimu hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Japhet Justine (aliyenyanyua mkono) akipata maelezo ya maendeleo ya
matrekta na mashine ya kuvunia walizozitoa kama mkopo kwa Skimu ya
Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Japhet Justine akichukua kumbukumbu ya mandhari ya shamba lenye
ukubwa wa hekta 220 linalolimwa kwa ufadhili wa mkopo kutoka TADB.
Timu ya Ukaguzi ikiangalia mandhari ya mifereji inayotumia kumwagilia shamba hilo.
Timu ya Ukaguzi ikiangalia namna uongezaji wa thamani wa zao la mpunga unavyofanyika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Japhet Justine akioneshwa mfuko utakaotumika kufungashia mchele
unaozalishwa na Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo. Skimu hii imeweshwa kwa
mkopo unaotolewa na TADB.
TADB yaendelea kuchagiza mapinduzi ya kilimo katika Skimu ya Umwagiliaji Mombo Tanga
Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB) imeahidi kunyanyua kipato cha
wakulima wadogo wadogo kupitia ushirika wao kwa kuwapatia mikopo ya
gharama nafuu ili waweze kumudu gharama za uzalishaji.
Akizungumza
wakati wa ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji
katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema benki yake
imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuwapatia
mitaji itayowawezesha kununua zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza
uzalishaji kama ilivyoanishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo ya
Kilimo (ASDP 2).
Akizungumza kwa
niaba ya wakulima wa skimu hiyo, Katibu wa Skimu ya Umwagiliaji ya
Mombo, Bwana Sufian Mohamed aliishukuru serikali kupitia Benki ya
Maaendeleo ya kilimo kwa kuwapatia mkopo wa gharama nafuu ambao umeweza
kuwanufaisha jumla ya wakulima 429 kati yao wanawake wakiwa asilimia 54,
mkopo ambao umeboresha miundo mbinu ya skimu hiyo hali iliyowezesha
kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 1.9 hadi kufikia tani 6 kwa
hekta moja.
Skimu hiyo ya
Mombo mpaka sasa imenufaika na mkopo wa mbolea, mbegu bora pamoja na
trekta, mashine ya kuvunia na sasa Benki ya Kilimo ipo katika hatua ya
mwisho ya kuwapatia mashine ya kukobolea mchele ili waweze kuongeza
thamani ya zao la mpunga katika skimu hiyo
No comments :
Post a Comment