Mh. Naibu Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokelewa na
Kaimu Mkuu wa Taasisi Ya Ustawi wa Jamii Dkt Zena Mabeyo alipofika
kutembelea Taasisi hiyo.
Mh. Naibu Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile Akiongea na
watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
Mh Naibu Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akisikiliza ripoti ya utendaji kazi wa
Taasisi ya Ustawi wa Jamii kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Taasisi Dkt. Zena
Mabeyo.
Wajumbe wa menejimenti ya Taasisi
ya Ustawi wa Jamii wakimsikiliza Mh. Naibu waziri Dkt. Faustine
Ndugulile wakati alipokutana nao Jana.
Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb)
Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto leo
tarehe 27/09/2018 amefanya ziara katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikiwa
ni
miongoni mwa ziara za kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake
katika kuboresha utendaji kazi.
Dkt Ndugulile amefanya mkutano na
menejimenti, wafanyakazi pamoja na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa
Taasisi ya Ustawi wa Jamii ambapo pamoja na mambo mengine Mh Naibu
Waziri alisomewa taarifa ya maendeleo ya taasisi na mipango ya baadae.
“Nimeskia taarifa nzuri ya
maendeleo na mafanikio pamoja na changamoto za Taasisi, nawaagiza
viongozi kutatua changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wenu na sisi kama
serikali tutazifanyia kazi zile zinazotuhusu. Lengo letu ni kuhakikisha
kuwa huduma zinaendelea kutolewa kwa ubora na maslahi ya watumishi
yanaboreshwa”. Alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Mh. Naibu waziri Ndugulile
ametoa maagizo kwa menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kufanyia
kazi kwa muda mwezi mmoja tu,baadhi ya mambo ambayo ameona yanahitaji
ufumbuzi wa mapema ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika
Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
Katika kuhitimisha mkutano wake na
uongozi, wafanyakazi pamoja na serikali ya wanafunzi wa Taasisi, Mh.
Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amepongeza kazi nzuri inayofanywa na
watumishi na ameahidi wizara kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Ustawi
wa jamii katika kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wananchi.
Imetolewa na:
Benedict Nkwao
Afisa Uhusiano
Taasisi ya Ustawi wa Jamii
Dar es Salaam
No comments :
Post a Comment