Afisa
Tawala wa Wilaya ya Kasulu,Bw.Titus Mguha, mweye shati la kitenge
akishirikiana na Meneja wa Miradi ya Maji kutoka taasisi ya Poul Due
Jensen Foundation,Bw.Nils Thorup kukata utepe kuzindua mradi wa maji sai
na salama katika kata ya Zeze wilayani Kasulu ambao umetekelezwa na
Water Mission Tanzania, kwa udhamini wa taasisi ya Poul Due Jensen
Foundation.
Afisa
Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Bw.Titus Mguha (wa pili kutoka kulia)
akifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa kata ya Zeze
ambao umejengwa na taasisi ya Water Mission Tanzania,kwa udhamini wa
taasisi ya, Poul Due Jensen Foundation,wengine pichani ni Mkurugenzi wa
Water Mission Tanzania Benjamin Filskov (wa kwanza kushoto),Mkurugenzi
wa water Mission wa kanda ,Will Furlong (katikati) na Meneja wa Miradi
ya Maji kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,Bw.Nils Thorup
Baadhi ya wakazi wa Zeze wakicheza ngoma kufurahia kupata maji.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi wakifuatilia
matukio
Wakazi wa Kata ya Zeze iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, kuanzia
sasa wana uhakika wa kupata maji safi na salama kutokana na kuzinduliwa
kwa mradi mpya wa kusambaza maji katika eneo lao.Mradi huo wenye uwezo
wa kuhudumia watu karibu 5,100,umefanikishwa na Shirika lisilo la
Kiserikali la kimataifa la Water Missions International Tanzania.
---
Serikali ya Tanzania,Water Missions International Tanzania na Poul Due
Jensen Foundation ,kwa pamoja tunatambua kuwepo mahitaji ya maji safi
na salama katika kanda hii na tunashirikiana pamoja na jamii zinazoishi
maeneo ya miradi tumehakikisha tunaanzisha miradi endelevu ya maji safi
na salama ambayo imeleta suluhisho la tatizo hili kwenye nchi za
Afrika Mashariki.”
Aliendelea kusema “Tunayo furaha kusheherekea uzinduzi wa mradi wa maji
wa kata ya Zeze,ikiwa ni kuienzi,siku ya Niels Due Jensen,kutimiza miaka
75 ya kuzaliwa na miaka 50 ya kutoa mchango wake wa kuhudumia miradi ya
kijamii kupitia taasisi ya Poul Due Jensen Foundation na kampuni ya
Grundfos,”
Mwakilishi kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,ambaye ni Meneja
wa miradi ya maji,Bw. Nils Thorup alisema “Niels Due Jensen, mwenyewe
ndiye alitoa maagizo kuwa pesa za msaada kutoka taasisi yake zisaidie
kufanikisha miradi ya maji karibu na moja ya eneo lililopo karibu kambi
za wakimbizi nchini Tanzania”.Niels siku zote anasema kufanya kazi
peke yako mafanikio yake yana mipaka ila kushirikiana na watu wengi
kunaweza kufanikisha kila jambo.
Ni wakati wenu wakazi wa jamii ya Zeze kushirikiana kwa pamoja
kuhakikisha mradi huu tunaosheherekea kuzinduliwa kwake siku hii ya leo
unakuwa endelevu.Hakuna anayeweza kufanikisha hilo peke yake bali
unahitajika ushirikiano na mkifanikisha hilo mradi huu utanufaisha
Watoto wenu,wajukuu mpaka vizazi vya mbele vijavyo”.
Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania nchini,Bw.Benjamin Filskov,
alieleza jinsi taasisi hiyo ilivyofanikisha miradi mbalimbali ya maji
nchini Tanzania “Niels Due Jensen amekuwa mfano wa kuigwa kwangu kwa
kuwa ameniwezesha kuielewa vizuri miradi endelevu ya maji na jinsi ya
kuifanikisha.Ninayo furaha kuienzi dhamira yake hiyo kupitia mradi huu.”
Wakazi wa kata ya Zeze idadi yao inakaribia watu 5,100,ikiwemo watu
wengine zaidi 410 ambao wanakuja kwenye taasisi za kihuduma zilizopo
kwenye kata hiyo (Shule na Zahanati) ambao wanafanya idadi ya watu
kufikia 5,510.Kata ya Zeze inazo shule za msingi 2,shule ya sekondari
moja,zahati ndogo na makanisa.Wakazi wa Zeze wamekuwa wakipata maji
kwenye visima na wengi wao wamekuwa wakitayumia kwa kunywa bila kuyaweka
katika mazingira ya usafi zaidi.
Kwa upande wake,Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu,Titus Mguha ,amesema
mradi huu ni wa kihistoria kutokana na eneo hilo kuwa na changamoto ya
maji kwa muda nrefu “Kwa niaba ya Serikali napenda kuzishukuru taasisi
za Water Mission Tanzania, the Niels Due Jensen Foundation na Grundfos
kwa jitihada zao ambazo zimefanikisha wakazi wa eneo hili wanapata maji
safi na salama”alisema.
Alisema,kabla ya kuanzishwa mradi huu,wanawake walikuwa wakisafiri
umbali mrefu kutafuta maji na maji waliyokuwa wakiyapata hayakuwa salama
ambapo yalisababisha kuwepo kwa milipuko mbalimbali ya magonjwa kwenye
jamii hiyo.
Alitoa wito kwa wanufaika wa mradi huo kuwa sehemu ya mradi huo na siku
zote kuwa mstari wa mbele kulinda miundombinu ya mradi na kuwapa
ushirikiano wataalamu wanaosaidia kuufanikisha “Kama Serikali ya wilaya
tuko tayari kushirikiana na Water Mission Tanzania,kuhakikisha mradi huu
unakuwa endelevu katika eneo hili ambalo linakua kwa kasi,”alisema.
No comments :
Post a Comment