NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, leo Septemba 23,
2018 ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi ya miili 9 kati ya 224
waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha Mv. Nyerere pembezoni mwa ziwa Victoria
eneo la Bwisya, Ukara, Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza
Miili
hiyo 9 ni kati ya minne (4) ambayo haikuweza kutambuliwa na jamaa zao, na mingine
mitano iliyotambuliwa lakini ndugu zao wameonelea wazikwe pamoja chini ya usimamizi
wa serikali, amesema Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack
Kamwelwe, wakati akitoa taarifa ya maafa hayo.
Akitoa
taarifa ya maafa hayo, Mhandisi Kamwelwe alisema hadi leo Septemba 23, 2018
wakati wa mazishi ya wenzetu hao, imethibitishwa kuwa jumla ya watu 224
wamepoteza ,maisha kwenye ajali hiyo.” Alsiema na kufafanua kuwa
Wanawake
(watu wazima) walikuwa 126, wanaume (watu wazima) walikuwa 71, watoto wa kike 17,
watoto wa kiume 10na hivyo kufanya jumla ya watu 224 waliopoteza maisha.”
Alisema.
Alizungumza
saa chache kabla ya mazishi hayo, Waziri Mkuu alisema,uchunhguzi wa awali
unaonyesha kivuko hicho kilipata ajali kutokana na kubeba uzito kupita kiasi,
ambapo alisema wakati kivuko kina uwezo wa kubeba watu 101, siku hiyo kilibeba
watu zaidi ya 224.
Akitoa
historia ya kivuko hicho cha Mv Nyerere, Waziri Kamwelwe alisema, kivuko cha Mv
Nyerere kilitengenzwa rasmi 2004 na kikaanza kufanya kazi, 2013 kikafanyiwa
ukarabati mkubwa na kurudishwa katika upya, mwaka 2015 kivuko kilifanyiwa
ukarabati tena.
“Tuliona
injini zimechakaa kidogo mwak 2017 tulinunua injini mpya 2 na gea box zake zilifungwa
kwa hiyo kivuko kilikuwa katika hali nzuri.
“Kivuko
kilikuwa na uwezo wa kubeba tani 25,
magari matatu na mizig” Alisema.
Alisema
kivuko hicho kilipinduka siku ya Alhamisi Septemba 20, 2018 majira ya saa 7:48 na
ilipofika saa 8:40 mchana taarifa za kutokea kwa ajali hiyo zilipelekwa ofisini
kwa mkuu wa mkoa na haraka Mkuu wa Mkoa akiwa na kamati yake ya ulizni na
usalama walielekea eneo la tukio.
“Tunawashukuru
wananchi wa hapa kwani baada tu ya kutokea ajali walianza kufanya kazi ya uokoaji na kupatikana
miili 43 na kuokoa watu wengine kadhaa.” Alsiema.
Waziri
Mkuu Mhe. Majaliwa amesema zoezi la uokoaji litaendelea nay eye mwenyewe
binafsi atabaki huko huko Ukara kusimamia zoezi hilo na kwamba serikali itaunda
Tume ya uchunguzi itakayohusisha wataalamu na vyombo vya dola ili kuchunguza
chanzo cha ajali ili watakaobainika waweze kuchukuliwa hatua’ Waziri Mkuu.
Alisema
serikali inafanya mpango wa kuleta kivuko kingine cha dharura Mv Nyahunge ili
kiweze kutoa huduma kwa wananchi.
Wakati
huo huo, serikali imetangaza namba ya Tigopesa kwa jina la RAS
Mwanza-0677030000. Na hadi sasa tayari zimekusanywa shilingi milioni 190 za
rambirambi hadi kufikia siku ya Septemba 23, 2018.
Aidha serikali pia imefungua akaunti maalum ya benki yenye jina MAAFA MV NYERERE, namba 31110057246
No comments :
Post a Comment