Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile
akikagua moja ya machine mpya ya X-ray ya kisasa ambayo iko tayari
kutumika. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious
Boniface.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akipata maelezo ya
hatua iliyofikiwa katika usimikaji wa mashine ya CT Scan, wengine ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu
(MOI) Dkt Respicious Boniface pamoja na viongozi waandamizi wa taasisi
hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile Dkt Ndugulile
akimjulia hali mtoto anayepata Huduma katika Taasisi ya MOI
Mtaalamu wa viungo bandia wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Deus David
akitoa ufafanuzi kwa Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile kuhusu namna viungo bandia
vinavyotengenezwa na kufanya kazi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na
moja ya mgonjwa ambaye anatengenezewa kiungo bandia MOI ili kubainisha
changamoto zilizopo zinazomkabili mgonjwa huyo.
(Picha zote na MOI
……………………
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile leo ametembelea na
kukagua hali ya utoaji wa huduma katika baadhi ya vitengo katika
Taasisi ya MOI na kukagua usimikaji wa mitambo ya kisasa katika kitengo
cha radiolojia yenye
thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 5.6 .
“Lengo la ziara yangu ni kukagua
maendeleo ya usimikaji wa mitambo hii ya kisasa ya MRI, CT SCAN, X-ray,
Ultra sound, nimeona na kujiridhisha imekamilika kwa asilimia 99% .
Naomba niwaelekeze mkamilishe mambo machache yaliyobaki ndani ya wiki
hii ili wiki ijayo wagonjwa waanze kupata huduma hapa”. Alisema Dkt
Ndugulile.
Pia, Dkt Ndugulule ametembelea
vitengo vya mazoezi tiba pamoja na utengenezaji wa viungo bandia ambapo
amekagua na kujiaonea hali ya utoaji huduma na kujiridhisha kwamba
huduma zimeboreka katika kipindi cha miaka 3 ya Serikali ya awamu ya
tano na kwa sasa watanzania wanapata huduma kwa wakati ijapokuwa kuna
changamoto chache ambazo Serikali inazishughulikia.
Aidha, Dkt Ndugulile ameupongeza
uongozi wa MOI kwa kuhakikisha usimikaji wa Mitambao unafanyika kwa
wakati na hali ya utoaji huduma ni nzuri na ya kuridhisha kwani wagonjwa
wamekuwa wakipata changamoto ya kwenda nje ya MOI kufuata vipimo hivyo.
Akitoa taarifa ya hali ya utoaji
huduma na usimikaji wa mitambo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt
Respicious Boniface amemueleza Dkt Ndugulile kwamba hali ya utoaji wa
huduma ni nzuri, wagonjwa wanapata huduma stahiki kwa wakati na idadi ya
wagonjwa wanaopata huduma imeongezeka maradufu baada ya eneo la kutolea
huduma kuboreshwa.
“Mhe. Naibu Waziri, hali ya utoaji
huduma katika taasisi yetu ni nzuri, idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa
upasuaji imeongezeka na kufikia 700-900 kwa mwezi kutoka 500 kutokana
ongezeko la vyumba 2 vya upasuaji katika jengo hili, awali tulikua na
vyumba 6 sasa vimekuwa 8, hii nikutokana na uwekezaji uliofanywa na
Serikali hii ya awamu ya 5 inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli”
alisema Dkt Boniface
Akihitimisha yake Dkt Ndugulile
amesema ni adhma ya Serikali kuhakikisha huduma zote zinapatikana hapa
nchini hivyo ni vyema kama kuna kifaa chochote kinachohitajika taarifa
itolewe Wizarani ili kifaa hicho kiwekwe kwenye mpango na bajeti na
kununuliwa kwani utaalamu na weledi upo wakutosha.
No comments :
Post a Comment