Ofisa wa Huduma kwa wateja wa
Benki ya NBC, Pili Salum akizungumza na watoto wa Shule ya Msingi Nyanza
wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini
yanayoendelea katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.
Ofisa Mahusiano ya Wateja wa Benki
ya NBC, Esther Kahabi akizungumza na wakazi wa Geita pamoja na
wafanyakazi wa migodini wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji
kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya CCM Kalangalala
mjini Geita.
Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Benki
ya NBC, Japhet Mazumira (kushoto) akizungumza na kikundi cha
wajasiriamali wadogo wadogo mafundi viatu walemavu baada ya kutembelea
katika banda lao wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye
Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani
Geita.
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC,
Joseph Boaz (kulia) akizungumza na wakazi wa Geita pamoja na wafanyakazi
wa migodini wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta
ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita.
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC,
William Kallaghe (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma
mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa Naibu Waziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo (kushoto) wakati naibu waziri huyo alipokwenda kuzindua
rasmi maonyesho ya kwanza ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya
Madini Mkoani Geita juzi. NBC ilikuwa ni mdhamini mkuu wa maonyesho
hayo. Wengine kutoka kulia ni Meneja wa NBC Geita, Martin Nkanda,
Meneja wa Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira na Mkuu wa Kitengo cha Wateja
Wadogo na wa Kati, Evance Luhimbo
Meneja Uhusiano wa Benki ya NBC,
William Kallaghe (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi
Gabriel Robert (wapili kulia) baada ya kutembelea katika banda la Benki
hiyo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Teknolojia na uwekezaji kwenye
sekta ya madini yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Kalangalala jijini
Geita juzi. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonyesho,
Chacha Wambura na Meneja wa NBC Geita, Martin Nkanda.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi
Gabriel Robert (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wapili
kulia) na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe
wakitembelea moja ya mabanda ya wajasiriamali katika maonyesho ya
Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini mjini Geita jana. NBC
ilikuwa ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
No comments :
Post a Comment