Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
KUMEIBUKA
matangazo kwenye mtandao wa FACEBOOK yanayosema kwamba Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa ameshiriki sherehe ya uzinduzi wa tovuti ya www.boreshamaisha.ml ambayo inatoa mikopo ndani ya dakika 45.
Waliofungua ukurasa huo wa FACECOOK, hawana uhusiano wowote na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tovuti hii yawww.boreshamaisha.ml inaonesha
ni ya Malaysia wala siyo ya Tanzania. Wanasema wanatoa mikopo hiyo
kutoka mfuko wa VICOBA TANZANIA ambao umeanzishwa katika mfumo wa
intaneti pekee (online). Wanadai wanatumia mawasiliano ya teknolojia kwa
uchukuzi wa haraka kupitia tovuti kwa lengo la kurahisisha upatikanaji
wa mikopo kwa kila Mtanzania popote alipo.
Wafunguaji wa
akaunti hiyo, wametumia jina la Kassim Majaliwa na wameweka picha yake
akiwa Bungeni. Wanadai kwamba Waziri Mkuu alipokea barua kutoka vyama
vya upinzani wakilalamika kwamba utoaji wa mikopo hiyo online kutoka
kwenye mfuko waVICOBA TANZANIA ni rushwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka
2020.
Pia wanadai
kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na viongozi wengine wamechangia
fedha zao kwenye mfuko huo wa kijamii unaolenga kuwapatia Watanzania
wote mikopo bila ubaguzi wa aina yoyote kwamba alishiriki uzinduzi wa
tovuti hiyo.
Kwa taarifa hii
ya umma, tunapenda kuujulisha umma wa Watanzania kwamba Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa hajashiriki uzinduzi wa tovuti hiyo, hana uhusiano
wowote na watu hao na wala hana akaunti ya facebook inayohamasisha
Watanzania wapate mikopo kwa dakika 45 kupitia njia ya mtandao.
Tunawaomba
Watanzania wajiepushe na akaunti hiyo ya FACEBOOK kwa kuwa si halali na
haina nia njema kwa watumiaji. Aidha, hiyo si akaunti ya Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na wala Ofisi ya Waziri Mkuu haijawahi kuunda akaunti ya
mtandao yenye jina lake kwa matumizi yake binafsi au ya ofisi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
- L. P. 980,
41193 – DODOMA.
JUMATANO, SEPTEMBA 19, 2018.
No comments :
Post a Comment