Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ,Bwana William Erio akiwa kwenye
mazungumzo na Menejimenti ya Benki ya CRDB ofisini kwake makao makuu
jijini DSM ambapo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali ya kuimairisha
mahusiano baina yao.
Viongozi wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) na viongozi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha
ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kwenye makao makuu ya
NSSF ,katikati Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio na pembeni
yake ni mkurugenzi mkuu wa CRDB Charles Kimei na pembeni ni viongozi
mbalimbali wa CRDB na NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA
,Bwana Usman Imam Isiaka akielezea jambo wakati wa mazungmzo yake na
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana
William Erio leo katika makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya
NMB Bi.Ineke Bussemaker akipongezana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio (Kulia) mara baada
ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao ofisini kwake jijini Dar es
Salaam. Wa kwanza kushoto ni Bwana Miichael Mungure amabaye ni MKuu wa
kitengo cha akaunti na
malipo(NMB), wa kwanza kulia ni Richard Mtapa
ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi za Serikali(NMB)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio amefanya mazungumzo
na Menejimenti ya baadhi ya Taasisi tatu za Kibenki hapa nchini ambazo
ni NMB,CRDB na UBA kwa lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya
kibiashara.
Katika mkutano huo wameweza
kuzungumza masuala mbali mbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano
utakaowezesha kukuza maendeleo katika sekta ya uchumi kupitia Benki zao
na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF.
Wakurugenzi wakuu hao ni pamoja
na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwana Charles Kimei,Bwana
Usman Imam Isiaka Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker.
No comments :
Post a Comment