Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe.
Stansalus Nyongo akitembelea baadhi ya mabanda katika maonesho
Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita.

Stansalus Nyongo akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho
Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita, ambapo
alisisitiza kuwa Ifikapo 2025 Sekta ya Madini Ichangie zaidi ya asilimia
10 katika pato la taifa.

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho Teknolojia
na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita ambapo alisisitiza
Serikali ya awamu ya tano itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya
maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya
teknolojia ya Dhahabu Mkoani Geita ambapo alimshukuru Mhe. Rais Dkt.
John Magufuli kwa kuwa mtetezi namba moja katika sekta ya madini.
Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe.
Stansalus Nyongo akiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi
wa maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita.
Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe.
Stansalus Nyongo akiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi
wa maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita
Naibu Waziri Wizara ya Madini Mhe.
Stansalus Nyongo akiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi rasmi
wa maonesho Teknolojia na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO, GEITA
Serikali imesema itahakikisha mpaka kufikia mwaka 2025 Sekta ya madini iwe inachangia zaidi ya asilimia 10 katika pato la taifa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Nishati, Mhe. Stanslaus Nyongo wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya
Teknolojia bora ya dhahabu tarehe 26/09/2018 Mkoani Geita.
Mhe. Nyongo amesema kuwa katika
mwaka 2016/2017 sekta ya madini imechangia asilimia
nne tu katika pato
la taifa hivyo hii imechagiza serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha
wanafikia zaidi ya asilimia 10 ifikapo 2025.
“kwa ujumla sekta ya madini
imekuwa ikitoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa taifa letu na
maendeleo ya mtu mmojammoja nchini ingawa matarajio ya Serikali ni
mchango huu kuongezeka zaidi na hatimaye kuinufaisha zaidi nchi na
watanzania kwa ujumla”-Alisema Mhe. Nyongo.
Aidha, Mhe. Nyongo amesema kuwa
mbali na mchango huo Serikali itaendelea kuiimarisha Taasisi ya Jiolojia
Tanzania na kuendelea kutoa ushirikiano kwa wachimbaji wadogo ili
kuhakikisha wanafikia lengo lililotarajiwa ikiwemo kuwawekea mazingira
mazuri ya utekelezaji majukumu yao.
Mhe. Nyongo amesema kuwa Wizara ya
madini itashirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Geita ili kuhakikisha
kunakuwepo na soko la madini katika eneo hilo.
Pia Mhe. Nyongo aliwataka
wachimbaji wadogo wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu za
sekta ya madini na kuacha kujihusisha na utoroshaji wa madini au
kufanya biashara ya magendo ikiwemo kukwepa mrabaha na kodi za serikali
kwani kufanya hivyo ni kuihujumu nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuwa mtetezi namba moja katika sekta ya madini ili yawanufaishe
watanzania.
Mhandisi Gabriel amesema kuwa
anaishukuru serikali kwa kuzuia kaboni kusafirishwa nje ya mkoa kwani
baada ya katazo katika mwezi wa sita walipata kilo 115.8, kwa mwezi wa
saba walipata kilo 141 ya dhahabu na kwa mwezi wa nane wamepata kilo
157.4, tofauti na miezi ya nyumba kabla ya katazo hilo hii imewezesha
halmashauri kupata fedha yake na Serikali kuu kukusanya kodi.
Akiongea katika mkutano huo
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi amewathibitishi wananchi kuwa Serikali ya awamu ya tano
ipo kazini na kuna mambo yanatokea nchi hii hayajawahi kutokea tangu
Tanzania iumbwe.
No comments :
Post a Comment