Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu,
Mh. Abdallah Hamis Ulega, akizungumza na Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya
(EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt.
Amani Ngusani baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maalim Kilwa Kivinje
mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018 kupokea msaada wa boti mbili za doria
zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia
miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu,
Mh. Abdallah Hamis Ulega, akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Jumuiya ya
Ulaya (EU), Jenny Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania,
Dkt. Amani Ngusani kuelekea baharini kupokea msaada wa boti mbili za
doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia
miradi ya WWF nchini.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu,
Mh. Abdallah Hamis Ulega, Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Jenny
Correia Nunes, na Mkurugenzi Mkazi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusani
wakisaini makubaliano baada ya kupokea msaada wa boti mbili za doria
zenye thamani ya Shilingi Millioni 144 zilizotolewa na EU kupitia
miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya Kilwa Kivinje na Mafia katika
Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani Lindi Tarehe 26.7.2018
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Mh. Abdallah Hamis Ulega,
akizungumza akipokea mkataba kutoka Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya (EU),
Jenny Correia Nunes, baada ya kusaini makubaliano ya kupokea msaada wa
boti mbili za doria zenye thamani ya Shilingi Millioni 144
zilizotolewa na EU kupitia miradi ya WWF nchini kwa Wilaya mbili ya
Kilwa Kivinje na Mafia katika Viwanja wa Maalim Kilwa Kivinje mkoani
Lindi Tarehe 26.7.2018
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah HamisUlega amekabidhi boti mbili za doria kwa BMU za Kilwa Kivinje na Mafia. Zoezi hili limefanyika katika Wilaya ya Kilwa eneo is Kivinje. Boti hizo zina thamani ya fedha za Kitanzania milioni 144 ambazo zimefadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia miradi ya WWF.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah HamisUlega amekabidhi boti mbili za doria kwa BMU za Kilwa Kivinje na Mafia. Zoezi hili limefanyika katika Wilaya ya Kilwa eneo is Kivinje. Boti hizo zina thamani ya fedha za Kitanzania milioni 144 ambazo zimefadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia miradi ya WWF.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya
Bibi Jenny amesema wanafadhili miradi ya WWF hapa Tanzania yenye jumla
ya bilioni 7 za Kitanzania. Aidha, amefurahi kusikia kwa uvuvi wa mabomu
umepungua sana na hii ni sababu ya juhudi za serikali na wananchi wa
maeneo haya. Pia alisema wao wamenunua boti ila jukumu za kuzilinda ni
la Serikali ya Wilaya husika.
Naye Mkurugenzi wa WWF nchini
amesema wamepata taarifa kutoka kwa wavuvi kwamba sasa samaki
wanaongezeka na kupatikana kwa samaki ambao walishapotea na haya yote ni
kwa sababu ya kupungua kwa asilimia kubwa uvuvi wa mabomu.
Mhe Ulega Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi amesema Umoja wa Ulaya umenunua hizi boti kuunga mkono kati
kubwa inayofanywa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ya Serikali yake ya
awamu ya tano. Alisema amezunguka wilaya za Mkinga, Tanga Mjini, Muheza,
Pangani na Lindi kote huko wavuvi wanakiri samaki wameongezeka kwa
sasa.
Ukanda huu wa Pwani hauna
viwanda vya samaki na kumuomba Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kutafuta
wawekezaji kuja kuwekeza viwanda vya samaki katika mwambao wa bahari ya
Hindi, pia alimuomba kufadhili ujenzi wa soko la samaki Kilwa Kivinje.
Mhe. Ulega aliwaasa umoja wa vikundi vya BMU kutunza boti hizo na
kuwaagiza Wilaya kusimamia ulinzi wa boti hizo. Mwisho aliwaomba WWF
kuwaangalia BMU na wavuvi wa maeneo mengine kama Mkinga, Pangani, Lindi
Vijijini na Mkuranga kwani nao wana mahitaji ya boti kama hizi katika
ulinzi wa rasilimali zetu za bahari.
No comments :
Post a Comment