Thursday, September 27, 2018

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUFANYA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO BILA MALIPO KATIKA VIWANJA VYA HOSPITALI YA VIJIBWENI WILAYANI KIGAMBONI jkci

jkci
TAARIFA KWA UMMA
MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI
TAREHE 29/09/2018
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kwamba  itafanya  upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo katika  Hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia saa 2 (mbili) asubuhi. Wananchi wote mnakaribishwa.

Kauli mbiu: “Kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”.
Limetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya  Moyo Jakaya Kikwete

No comments :

Post a Comment