Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Paul Makonda leo ametoa miezi minne kwa waajiri wa Makampuni na
Mashirika kuhakikisha wanawaajiri watu wenye ulemavu Kama Sheria ya
Walemavu ya 2010 na Mikataba ya kimataifa ya mwaka 2006 iliyoridhiwa na
Tanzania mwaka 2009 sura ya 27 unavyowaaagiza kufanya hivyo.
RC Makonda amesema ifikapo Mwezi
January mwakani ataanza ziara ya kutembelea kwenye kila kampuni na
taasisi jijini humo kukagua Kama wametekeleza sheria na agizo hilo
ambapo watakaobainika kukaidi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Aidha RC Makonda amesema kitendo
cha kuwaajiri walemavu itapunguza ongezeko la ombaomba,ukatili, utupwaji
wa watoto wenye ulemavu, kuhamasisha walemavu kusoma pamoja na
kuwawezesha walemavu kuhudumia familia zao.
“Hatuwezi kuwa na ndugu zetu
wamesoma na wanasifa za kupata Kazi lakini tunawanyima matokeo yake
wengine wanaishia kujinyonga, kinamama wanatupa Watoto wenye ulemavu,
mila potovu zinaendelea kupoteza haki na mwisho wanabaki wakiwa Masikini
na kushindwa hata kumudu gharama za Matibabu, Jambo hili sio la
kufumbia macho” alisema Makonda
Kwa mujibu wa Sheria ya ajira kwa
watu wenye ulemavu No. 9 ya mwaka 2010 kifungu cha 31 inamtaka kila
mwajiri mwenye wafanyakazi zaidi ya 20 kuhakikisha 3% ya wafanyakazi ni
watu wenye ulemavu.
RAIS MAGUFULI AMEONYESHA DIRA KWA KUTOA KIPAOMBELE CHA AJIRA KWA WALEMAVU, NI WAKATI SASA KWA WAAJIRI KUTEKELEZA SHERIA.
No comments :
Post a Comment