Mgeni
rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti aliyemaliza
muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi
akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki ya CBA (hawapo
pichani) wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10
tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
NA
MWANDISHI WETU
MWENYEKITI
Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi ameitaka benki ya biashara ya CBA kuendelea
kuwawezesha watanzania, hususani wa chini wapatao milioni 7.5 kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
umaskini.
Dk.
Mengi alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya
benki hiyo mjini Dar es salaam ambapo yeye ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Pamoja
na historia ndefu ya benki hiyo ilivyoanzishwa na baadae kuhamishia makao yake
makuu mjini Nairobi, Kenya, Dk. Mengi alisema benki hiyo ina wajibu mkubwa wa
kuwezesha kundi kubwa la watanzania kuukataa umaskini.
Dk.
Mengi ambaye ametoa kitabu kinachoonesha jinsi ya kukabiliana na umaskini na
ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF,
amesema amevutiwa na mpango wa Benki hiyo wa kuwapatia mikopo watu wa kawaida
sana kupitia mpango wake wa kuweka akiba kupitia simu za mikononi ujulikanao
kama M- Pawa.
Alisema
anaamini kama benki imedhamiria na kujiamini wanaweza kujipatia mafanikio
makubwa kupitia falsafa ya ninaweza. Anasema njia ya dhamira ya kwamba mtu
anaweza hakuna cha maana kinachoweza kufanyika.
Mapema
viongozi mbalimbali na waalikwa wakizungumzia huduma ya CBA tawi la Tanzania
walisema kwamba inawasaidia sana hasa watu wa kipato cha chini na hivyo
wanajihakikishia maendeleo kupitia M-pawa.
Mapema
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo
Bw. Martin Mugambi, na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Tanzania Bw. Gift
Shoko walisema benki ya CBA yenye umri
wa miaka 56 barani Afrika ina wateja
zaidi ya milioni 35, na hapa nchini
imewekeza mtaji wa dola za kimarekani milioni 50.
Viongozi
hao wawili walisema kwa msisitizo mkubwa wanatoa huduma bora zinazounganisha
wananchi katika kupata mikopo na kuweka akiba.
Walisema
kwamba mipango yao ni kuimarisha huduma za wateja wadogo kwa kuwa wao ndio
tegemeo la kuinua uchumi wa Tanzania kupitia ujasirimali.
Tafrija
ya Maadhimisho hayo ilipambwa na mnada ulioendeshwa na Taasisi ya Doris Mollel
Foundation, wa kuchangisha fedha za kusaidia watoto njiti katika hospitali ya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, ambapo
jumla ya shilingi milioni 17.6 zilipatikana.
Mgeni
rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi katika picha ya
pamoja na meza kuu wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi ( wa pili
kushoto) katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania
Bw. Gift Shoko (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin
Mugambi (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Mauzo na Huduma Binafsi za Kibenki wa
benki ya CBA nchini Bi. Edditrice Temba.
Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin Mugambi akitoa salamu za benki hiyo kwa
wageni waalikwa pamoja na mgeni rasmi (hawapo pichani) wakati wa tafrija ya
maazimisho ya Benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania Bw. Gift Shoko akizungumza na wageni
waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa tafrija ya maazimisho ya
benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Huduma za Kibenki na Masoko wa benki ya CBA nchini, Bw. Julius Konyani akitoa
neno la shukrani kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa tafrija ya
maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA Tanzania Bw. Gift Shoko akikamkaribisha mgeni
rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye pia ni ambaye ni Mwenyekiti aliyemaliza
muda wake wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF Dk. Reginald Mengi kwenye
eneo maalum walipomuandalia wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji anayeshughulikia
Masoko Makao Makuu ya Benki ya CBA, Chris Pasha na Wa pili kushoto ni Mkuu wa
Huduma za Kibenki na Masoko wa benki ya CBA nchini, Julius Konyani.
Mgeni
rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi (katikati) akifurahi jambo
na Mkurugenzi wa Benki ya CBA nchini Vinoo Somaiya (kulia) wakati wa tafrija ya
maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya
CBA, Martin Mugambi.
Msanii
wa muziki wa Bongo Flava, Elias Barnaba 'Barnaba Classic' akitoa burudani ya
wimbo maalum wa kupongeza benki ya hiyo tafrija ya kutimiza miaka 10 tangu
kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wageni waalikwa waliohudhuria tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake tena hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wageni waalikwa waliohudhuria tafrija ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza
miaka 10 tangu kuanzishwa kwake tena hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumza
jambo na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa tafrija ya maazimisho ya Benki ya
CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Martin Mugambi katika picha ya pamoja na baadhi
ya wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo
kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa benki ya CBA nchini katika picha ya pamoja wakati wa wa tafrija
ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake tena hapa
nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wateja wa Benki ya CBA nchini, Allan Makame akitoa ushuhuda jinsi
alivyofanikiwa kibiashara kutokana na mikopo yenye gharama nafuu inayotolewa na
benki hiyo wakati wa tafrija ya maazimisho ya benki hiyo kutimiza miaka 10
tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akizungumzia
kazi za taasisi yake kabla ya kuendesha mnada wa vitu ili kuchangisha fedha za
kusaidia watoto njiti katika hospitali ya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro,
ambapo jumla ya shilingi milioni 17.6 zilipatikana wakati wa tafrija ya
maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Taasisi
ya Doris Mollel Foundation ikiendesha mnada wa vitu ili kuchangisha fedha za
kusaidia watoto njiti katika hospitali ya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro,
ambapo jumla ya shilingi milioni 17.6 zilipatikana wakati wa tafrija ya
maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake tena hapa
nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugeni
wa Benki ya CBA, Suzane Ndomba akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja
aliyeshiriki mchezo wa gofu katika kusheherekea maazimisho ya benki hiyo
kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini iliyofanyika katika hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa benki ya CBA wakicheza ‘kwaito’ wakati wa tafrija
ya maazimisho ya Benki ya CBA kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake hapa
nchini iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment