Waumini
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Kusini Mtaa wa Mwapemba
wakiwa katika ibada ya kuwekwa jiwe la msingi wa ujenzi wa kanisa na uzinduzi
wa mtaa iliyofanyika jana katika kanisa hilo lililopo Temeke jijini Dar es
Salaam.
NA
ANNA NKINDA
WAUMINI wa Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wametakiwa kumtegemea
Mungu katika maisha yao na kuacha tabia ya kuhama hama makanisa kwa
kudhani kuwa huko wanakokwenda ni kuzuri zaidi ya mahali walipotoka.
Rai hiyo imetolewa
jana na Mkuu wa Jimbo la Kusini kutoka Dayosisi ya Mashariki na Pwani
Mchungaji Andrew King’homella wakati wa ibada ya kuwekwa kwa jiwe la
msingi pamoja na uzinduzi wa Mtaa wa Mwapemba uliopo wilaya ya Temeke jijini
Dar es Salaam.
Mchungaji
King’homella alisema Mungu yuko kila mahali jambo la muhimu ni kwa
mkristo kusoma biblia na kuifahamu, kumwomba Mungu katika
roho na kweli na kumsikiliza Mungu kwa kufanya hivyo Mungu atasikia na
kujibu maombi yake.
“Wakristo wengi
wamekuwa ni watu wa kuvunjika moyo hasa wanapokutana na matatizo mbalimbali
wanafikiri kwa kuhama makanisa shida zao zitakwenda kumalizika, wanasahau kuwa
Mungu yupo hata pale wanapoabudu”.
“Ukimtegemea Mungu
kwa neema yake hata kama unateseka kwa magonjwa na matatizo mengi wakati wako
ukifikaa atakuponya haijalishi uko mahali gani”, alisisitiza Mchungaji
King’homella .
Akisoma risala ya
ujenzi wa kanisa hiko Mwenyekiti wa Kamati ya majengo David Kisai alisema mtaa
huo ulianza mwaka mwezi wa kumi mwaka 2013 kwa kuwa na waumini 13 kati
ya hao watu wazima tisa na watoto wa nne ambapo ibada zilikuwa
zinafanyika katika moja ya nyumba ya muumini. Hivi sasa kuna jumla ya
waumini 187 kati ya hao watu wazima 127 na watoto 60.
“Jengo hili
likikamilika litakuwa na uwezo wa kuchukuwa waumini 300 katika ibada moja na
litakuwa na vyumba vitano vya ofisi ambavyo ni ofisi za mchungaji, Mwinjilisti,
Parish worker na ofisi nyingine mbili zitatumika kwa matumizi mbalimbali ya
kanisa” alisema Kisai.
Ibada hiyo ilienda
sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ambapo jumla ya
shilingi milioni 25 zilipatikana huku malengo yakiwa ni kuchangisha milioni 50
fedha ambazo zitatumika kukamilisha ujenzi wa boma pamoja na kuezeka.
Mkuu
wa Jimbo la Kusini wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Mashariki na Pwani Mchungaji Andrew King’homella akiweka
jiwe na msingi la ujenzi wa
Kanisa na uzinduzi wa Mtaa wa Mwapemba
katika ibada iliyofanyika jana kwenye kanisa hilo lililopo Temeke jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Jimbo la Kusini wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Mashariki na Pwani Mchungaji Andrew King’homella akifanya maombi kabla ya kuweka jiwe na msingi la ujenzi wa Kanisa na uzinduzi wa Mtaa wa Mwapemba katika ibada iliyofanyika
jana kwenye kanisa hilo lililopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Waumini
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Kusini Mtaa wa Mwapemba
wakilizunguka kanisa lao huku wakiimba kabla ya kuanza kwa ibada ya kuwekwa
jiwe la msingi wa ujenzi wa kanisa na uzinduzi wa mtaa iliyofanyika jana katika
kanisa hilo lililopo Temeke jijini Dar es Salaam.

Kibao
cha jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Mashariki na Pwani Jimbo la Kusini Mtaa wa Mwapemba kama kinavyoonekana katika
picha.
Waumini
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Jimbo la Kusini Mtaa wa Mwapemba
wakilizunguka kanisa lao huku wakiimba kabla ya kuanza kwa ibada ya kuwekwa
jiwe la msingi wa ujenzi wa kanisa na uzinduzi wa mtaa iliyofanyika jana katika
kanisa hilo lililopo Temeke jijini Dar es Salaam.(PICHA NA ANNA NKINDA)





No comments :
Post a Comment