Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula
akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la Pili la
Tathmini na Ufuatiliaji lililoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo
Kikuu cha Calfonia cha Marekani lililofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Ofisi
ya Rais TAMISEMI Bw. Erick Kitali akisissitiza umuhimu wa Taasisi za
Serikali kushirikiana na Ofisi hiyo katika kujenga mifumo mbalimbali
ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi katika sekta ya afya
wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la Pili la Tathmini na Ufuatiliaji
lililoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Calfonia cha
Marekani lililofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula
akimkabidhi cheti cha ushiriki Afisa uhusiano wa Chuo Kikuu Mzumbe Bi.
Fatna Mfalingundi wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la Pili la
Tathmini na Ufuatiliaji lililoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo
Kikuu cha Calfonia cha Marekani lililofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula
akimkabidhi cheti cha ushiriki mkuu wa Shule ya Menejimenti na Utawala
Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Eliza Mwakasangula wakati wa hafla ya kufunga
Kongamano la Pili la Tathmini na Ufuatiliaji lililoandaliwa na Chuo
Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Calfonia cha Marekani lililofanyika
Jijini Dodoma.
Mmoja wa washiriki wa Kongamano la
Pili la Tathmini na Ufuatiliaji lililoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe na
Chuo Kikuu cha Calfonia cha Marekani akipokea cheti cha ushiriki kutoka
kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa anayeshughulikia Afya ( TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula kwa
lililofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula
(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa
Kongamano la Pili la Tathmini na Ufuatiliaji wakati wa hafla ya
kufunga Kongamano hilo lililoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu
cha Calfonia cha Marekani na kufanyika Jijini Dodoma .
Na; Mwandishi Wetu- Dodoma
Chuo Kikuu Mzumbe kimepongezwa kwa
kuendesha kwa ufanisi Kongamano la Pili la Tathmini na Ufuatiliaji
linalowaleta pamoja wataalamu wa sekta ya afya, wahadhiri na
wanafunzi
wa chuo hicho.
Akizungumza Jijini Dodoma wakati
akifunga Kongamano hilo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais , Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Afya,
Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa utaratibu wa kuwa na Kongamano hilo
utasaidia kuunganisha Taasisi za Serikali kwa kushirikiana na Chuo
Kikuu cha Mzumbe ili kutumia tafiti zinazofanywa katika kutatua
changamoto zilizopo katika sekta ya afya.
“Tunatarajia washiriki wa
kongamano hili kutumia taaluma zao kuleta matokeo makubwa katika maeneo
wanayofanyia kazi” alisisitiza Dkt. Chaula
Akifafanua zaidi amesema kuwa,
dhamira ya serikali ni kuona suala la tathmini na ufuatiliaji linapewa
mkazo katika maeneo yote ya kazi ili kuleta matokeo chanya
yatakayowanufaisha wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Erick Kitali amesema kuwa ni
muhimu kwa taasisi za serikali kuja pamoja na kushirikiana katika
kujenga mifumo mbalimbali itakayosaidia kuboresha maisha ya wananchi.
Aliongeza kuwa, kuna umuhimu
mkubwa wa kushirikiana katika kutekeleza masuala mbalimbali ya sekta ya
afya hasa katika suala la ujenzi wa mifumo kupitia katika mradi huo wa
Tathmini na Ufuatiliaji unaotekelezwa na Chuo hicho.
Kongamano la pili la tathmini na
ufuatiliaji limefanyika Jijini Dodoma na kuratibiwa na Chuo Kikuu Mzumbe
kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Calfonia cha Marekani ambapo Kongamano
hilo limewaleta pamaoja Wataalamu wa tafiti, Wanafunzi na Wahadhiri wa
Chuo hicho wakishirikiana na wataalamu kutoka chuo Kikuu cha Calfonia.
No comments :
Post a Comment