RAIS John Magufuli ametaja sababu
ya daraja juu (Fly Over) ya Tazara kuitwa jina la Ofisa Mtendaji wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick mfugale ‘Daraja
la Mfugale’.
Wakati akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa Daraja la Mfugale iliyofanyika leo tarehe 27 Septemba 2018
jijini Dar es Salaam, amesema uzalendo na uchapakazi wa Mhandisi
Mfugale tangu alipoanza kuitumikia nchi katika masuala ya
ujenzi, ndiyo
sababu ya daraja hilo kupewa jina lake.
“Watalaamu wetu nchini waige
mfano wa uchapakazi wa Mfugale, mfugale hakupendelewa ni haki yake, yako
mengi aliyofanya kwa ajili ya nchi ametanguliza utanzania badala ya
ubinafsi, wako wataalamu wetu wachache wamekuwa chanzo cha matatizo hapa
nchini,” amesema Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema imezoeleka
kwa majina ya wanasiasa kutumika katika madaraja na barabara mbalimbali,
lakini kwa sasa ameamua heshima hiyo kutoa kwa wataalamu wanaoshiriki
ujenzi wa barabara na madaraja.
“Pamoja na sifa zote zilizotajwa
hapa za kujenga daraja la Mkapa ambalo ni refu kuliko yaliyokuwepo
katika Afrika Mashariki na kati, akajenga daraja la umoja na madaraja
mengine,” amesema Rais Magufuli.
No comments :
Post a Comment