Mkutano
wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC), unaofanyika mjini Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 17
hadi 18 Agosti
2018, umemteua Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa
Tanzania kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha Agosti 2018
mpaka Agosti
2019.
Kufuatia
uteuzi huo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania atapewa rasmi jukumu la Uenyekiti wa SADC katika Mkutano mkuu ujao wa
39 utakaofanyika Tanzania mwezi Agosti 2019.
 |
| Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika
mjini Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018. |
 |
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akifuatilia ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na
Serikali mjini Windhoek, Namibia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afika Kusini, Mhe Lindiwe Sisuli.
 |
| Kulia
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof Adolf Mkenda akifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano wa
Wakuu wa Nchi na Serikali mjini Windhoek, Namibia. |
|
 |
| Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena L.
Tax akitoa hotua ya ufunguzi wa mkutano pamoja na taarifa ya mwaka ya
utekelezaji wa Jumuiya ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi
waliomaliza muda na nchi wanachama kwa ushirikiano walioutoa katika
utekelezaji wa malengo na mipango mbalimbali ya kanda. |
 |
| Rais
wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda,
Mhe. Cyril Ramaphosa akikabidhi nafasi ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya
na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Hage Geingob. |
 |
| Mwenyekiti
wa SADC na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akihutubia mara baada ya
kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa SADC mjini Windhoek, Namibia ambapo
aliishukuru Serikali ya Afrika kusini kwa uongozi mahiri kwa kipindi
chote cha uongozi wake na aliahidi kushirikiana na wanachama wote katika
kuiletea kanda maendeleo na kupunguza umasikini. |
 |
| Wanafunzi
walioshinda shindano la insha wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu
Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Cyril
Ramaphosa njini Windhoek ,Namibia. |
 |
| Sehemu
nyingine ya Wanafunzi walioshinda shindano la insha wakiwa katika picha
ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena L. Tax na
Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Cyril Ramaphosa njini Windhoek ,Namibia. |
 |
Waandishi
wa habari walioshinda shindano la mwandishi bora wa SADC katika radio,
gazeti na televisheni wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji
wa SADC, Dkt. Stergomena Tax na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Cyril Ramaphosa
njini Windhoek ,Namibia.
 |
Kutoka
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SMZ), Bw. Ali
Juma Khamis pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikaiano wa Afrika Mashariki , Balozi
Innocent Shiyo wakifuatilia mkutano.
 |
| Kutoka
Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Joseph Nyamhanga pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu wakifuatilia mkutano. |
|
|
 |
| Wa
pili kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Bw. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Agness
kayola (kulia) wakifuatilia mkutano. |
 |
| Kutoka
kustoto ni Balozi wa Tanzania nchini Namibia mwenye makazi yake nchini
Afrika Kusini, Mhe. Sylisvester Ambokile na Naibu Mwanasheria Mkuu, Bw.
Evaristo Longopa wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano. |
 |
| Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania ukufuatilia mkutano. |
 |
| Sehemu nyingine ya ujumbe huo ukifuatilia mkutano. |
 |
| Waasisi
wa SADC wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Tiafa wa Namibia na wimbo wa
SADC ukipigwa, kushoto ni Rais mstaafu wa kwanza wa Jamhuri ya
Namibia, Mhe. Sam Nujoma na kulia kwake ni Rais wa mstaafu wa kwanza wa
Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Joaquim Chissano. |
 |
| Wake za Waheshimiwa marais walifuatilia hafla ufunguzi wa Mkutano |
 |
| Picha ya pamoja |
No comments :
Post a Comment