Friday, August 24, 2018

POLISI WAGUNDUA BARABARA YA CHINI YA ARDHI INAYOTUMIKA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA


barabara
BARABARA ya chini ya ardhi inayotumika kusafirisha mihadarati kutoka Mexico hadi Marekani imegunduliwa katika Jimbo la Arizona.
Barabara hiyo iliyokuwa ikitumika kwa siri na wahalifu imegunduliwa na mamlaka nchini Marekani .
Mamlaka nchini Marekani iliigundua barabara hiyo kwenye nyumba moja iliyoko maeneo ya San Luis ambayo inapitia chini ya mpaka hadi kwenye nyumba moja iliyoko San Luis Rio Colorado.
Barabara hiyo ina urefu wa mita 180 iligundulika baada ya mthumiwa anayefahamika kwa jina la Ivan Lopez kuwaelekeza polisi kuhusu barabara hiyo.
Chanzo: BBC Swahili

No comments :

Post a Comment