Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(World Meteorological Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa
Mataifa inayoshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa
yanayohusiana na ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na namna mifumo
hii inavyoathiri mazingira yetu. Shirika hufanya kazi zake kupitia
...
taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama (National Meteorolgical and
Hydrological Services – NMHSs) ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) ni mwakilishi rasmi wa shirika hili hapa nchini.
Katibu Mkuu wa WMO amefanya ziara
katika ofisi za TMA ili kujionea shughuli za hali ya hewa na namna
ambavyo WMO inaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali yahusuyo hali ya
hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa vya hali ya hewa. Aidha
aliipongeza TMA katika juhudi zake za utekelezaji wa programu za WMO
na kuzisaidia nchi zingine za Afrika. Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni
taasisi ya mfano Afrika katika utoaji wa huduma bora za hali ya hewa
Nae mkurugenzi mkuu wa TMA dkt.
Agnes Kijazi aliwashukuru Prof. Taalas kwa uamuzi wake wakutembelea
Tanzania na alimuahidi kuwa Tanzania kupitia TMA itaendelea kutekeleza
makubaliano yote ya kimataifa yahusuo huduma za hali ya hewa ikiwa ni
pamoja na utekelezaji wa program za WMO
Ikumbukwe kuwa WMO huratibu na
kusaidia katika kuboresha huduma za hali ya hewa katika nchi kama vile
kuanzisha mitandao ya ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuweka miongozo
inayosaidia utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa viwango na ubora wa
kimataifa n.k
Kupitia WMO Tanzania na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania imenufaika na kuongezewa uwezo kupitia mafunzo,
miundombinu ya hali ya hewa, hushiriki kikamilifu katika shughuli za
jopo la sayansi la kimataifa la ufuatiliaji wa mabadiliko ya hali ya
hewa (Intergovernmental Pannel on Climate Change – IPCC). Pia, kushiriki
katika shughuli za kongamano la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
masuala ya mabadiliko ya tabia nchi hasa masuala ya kisera (United
Nations Framework for Climate Change Conference – UNFCCC) ambapo
mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea Tanzania hujumuishwa katika
makubaliano ya kimataifa kwa ajili ya utekelezaji kimataifa na kitaifa
kwa faida ya nchi yetu.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments :
Post a Comment