Friday, August 24, 2018

KAMATI YA BUNGE MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA KUKUTANA NA WATENDAJI WA JESHI LA MAGEREZA LEO JIJINI DODOMA


PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kabla ya kuingia kwenye Kikao cha Kamati ya Bunge Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama kinachofanyika leo Agosti 24, 2018, jijini Dodoma. Kamati hiyo inakutana na watendaji wa Jeshi la Magereza na Idara ya Wakimbizi.
PIX 2
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati ya Bunge Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama leo Agosti 24, 2018, jijini Dodoma.
PIX 3
Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola kama inavyoonekana katika picha kabla ya kushiriki kikao kazi cha Kamati ya Bunge Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama.
PIX 4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola(katikati) akijadiliana na Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kuanza kwa kikao kazi cha Kamati ya Bunge Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama, leo Agosti 24, 2018 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dododma
Picha zote na Jeshi la Magereza

No comments :

Post a Comment