NA
MHT
SHIRIKA la Hali ya Hewa Duniani (World
Meteorological Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa Mataifa
inayoshughulikia masuala ya ushirikiano wa kimataifa yanayohusiana na
ufuatiliaji wa mifumo ya hali ya hewa na namna mifumo hii inavyoathiri
mazingira yetu. Shirika hufanya kazi zake kupitia taasisi za hali ya hewa za
nchi wanachama (National Meteorolgical and Hydrological Services - NMHSs)
ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni mwakilishi rasmi wa shirika
hili hapa nchini.
Katibu Mkuu wa WMO amefanya ziara katika ofisi za TMA
ili kujionea shughuli za hali ya hewa na namna ambavyo WMO inaweza kusaidia
katika maeneo mbalimbali yahusuyo hali ya hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa
vya hali ya hewa. Aidha aliipongeza TMA katika juhudi zake za utekelezaji wa programu za WMO na kuzisaidia nchi zingine
za Afrika. Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni taasisi ya mfano Afrika katika
utoaji wa huduma bora za hali ya hewa
Nae mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi aliwashukuru Prof. Taalas kwa uamuzi wake
wakutembelea Tanzania na alimuahidi kuwa Tanzania kupitia TMA itaendelea
kutekeleza makubaliano yote ya kimataifa yahusuo huduma za hali ya hewa ikiwa
ni pamoja na utekelezaji wa program za WMO
Ikumbukwe kuwa WMO huratibu na kusaidia
katika kuboresha huduma za hali ya hewa katika nchi kama vile kuanzisha
mitandao ya ufuatiliaji wa hali ya hewa, kuweka miongozo inayosaidia utoaji wa
huduma za hali ya hewa kwa viwango na ubora wa kimataifa n.k
Kupitia WMO Tanzania na Mamlaka ya Hali
ya Hewa Tanzania imenufaika na kuongezewa uwezo kupitia mafunzo, miundombinu ya
hali ya hewa, hushiriki kikamilifu katika
shughuli za jopo la sayansi la kimataifa la ufuatiliaji wa mabadiliko ya hali
ya hewa (Intergovernmental Pannel on Climate Change - IPCC). Pia, kushiriki
katika shughuli za kongamano la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya
mabadiliko ya tabia nchi hasa masuala ya kisera (United Nations Framework for
Climate Change Conference - UNFCCC) ambapo mabadiliko ya hali ya hewa
yanayotokea Tanzania hujumuishwa katika makubaliano ya kimataifa kwa ajili ya
utekelezaji kimataifa na kitaifa kwa faida ya nchi yetu.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akichangia
jambo baada ya kupata maelezo ya mfumo wa kisasa utoaji taarifa za hali ya hewa
kwa usafiri wa anga wakati alipotemebelea ofisi za hali ya hewa zilizopo katika
Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere. hewa.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo
ya namna ya kuwaandikisha wakulima katika mfumo wa utoajia taarifa za hali ya
hewa kilimo kupitia simu za mkononi uitwao FARMSMS kutoka kwa meneja wa huduma
za matumizi ya taarifa za hali ya hewa Bw, Isack Yonah
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo
kutoka kwa meneja wa mtandao wa vituo vya hali ya hewa nchini Bi. Hellen Msemo
kuhusiana na studio ya TMA inayohusika katika kurekodi utabiri wa hali ya hewa
wa kila siku.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata maelezo
kutoka kwa meneja wa mtandao wa vituo vya hali ya hewa nchini Bi. Hellen Msemo
kuhusiana na studio ya TMA inayohusika katika kurekodi utabiri wa hali ya hewa
wa kila siku.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akipata
maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA Bw. Chuki Sangalugembe
kuhusiana na mtambo mkubwa wa kompyuta (Computer Cluster)
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akishuhudia na
kushiriki mkutano wa kuandaa utabiri wa siku unaofuatilia hali mbaya ya hewa kwa
nchi za Afrika mashariki zilizoko katika Bonde la Ziwa Victoria.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas katika picha ya
pamoja na menejimenti ya TMA
No comments :
Post a Comment