Pages
Friday, August 31, 2018
TAASISI YA MOYO YAANZISHA KITENGO CHA HUDUMA KWA MTEJA (CUSTOMER CARE)
Mkurugenzi
Idara ya Uuguzi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya (kulia) akitoa mada ya namna ya kupokea wagonjwa kwa waajiriwa wa
kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer
care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo
mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo
Jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi
wa kampuni ya Professional Cleaner ambaye ni mmoja kati ya watoa huduma kwa
mteja (customer care) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Khadija Abeid akielezea
namna ambavyo atakua akitoa huduma bora kwa wateja wakati wa mafunzo mafupi ya
utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Jijini Dar es Salaam.(Picha
na:
Genofeva Matemu)
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LAELEZA MATARAJIO NA MALENGO YAKE KWA MWAKA 2018/2019
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akielezea masuala mbalimbali yanayohusu matarajio na malengo ya shirika hilo, kwa mwaka 2018/2019. Kushoto ni Postamasta Mkuu wa shirika, Hassan Mwang’ombe. |
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia
Madulesi, akizungumza wakati akiwakaribisha waandishi wa habari katika
mkutano ambao Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk.
Haruni Kondo, alielezea mambo mbalimbali yanayohusu matarajio na
malengo ya shirika hilo, kwa mwaka 2018/2019, jijini Dar es Salaam leo.
Kulia ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe na kushoto ni Kaimu Meneja
Mkuu Rasilimali za Shirika Macrice Mbodo.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua
taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta
Tanzania, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya wapiga picha na waandishi wa habari, wakichukua taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Baadhi ya wapiga waandishi wa habari, wakisikiliza taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi katika mkutano huo.
Postamasta
Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akizungumza katika mkutano huo, wakati
alipoelezea kuhusu duka la Shirika la kwenye mtandao kwamba sasa tayari
linafanya kazi na kuwataka wananchi kulitumia kwa kuweka bidhaa zao ili
kuweza kuuza ndani na nje ya nchi. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.
Maofisa wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC),wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Hassan Mwang'ombe, alipokuwa akizungumza katika mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo.
Postamasta
Mkuu, Hassan Mwang'ombe,akizungumza wakati alipokuwa akijibu maswali
yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo,jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo.
MUHIMBILI WATOA KIWANJA CHA UJENZI WA KITUO CHA POLISI MLOGANZILA
Kaimu
Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe wakibadilishana
nyaraka baada ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la
Polisi eneo la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa
kituo cha Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es
Salaam.
Kaimu
Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili Prof. Andrea Pembe wakisaini
makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo la ekari mbili
katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.Makubalino
hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam
Kaimu
Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi shirikishi Mhimbili Prof. Andrea Pembe wakizungumza baada
ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo la
ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha
Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.(Picha
na Jeshi la Polisi)
Kaimu
Kamishna wa Fedha na Lojistiki, DCP Leonard Paul na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi shirikishi Mhimbili Prof. Andrea Pembe wakionyesha nyaraka
baada ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la Polisi eneo
la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha
Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
Maofisa
kutoka Makao Makuu ya Polisi na viongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
shirikishi Mhimbili wakiwa katika picha
ya pamoja baada ya kusaini makubaliano ambapo Chuo hicho kimelipatia Jeshi la
Polisi eneo la ekari mbili katika Kampasi ya Mloganzila kwa ajili ya ujenzi wa
kituo cha Polisi.Makubalino hayo yalisainiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es
Salaam.(PICHA NA JESHI LA POLISI)
NAIBU WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA SEKTA BINAFSI KWA MCHANGO MKUBWA KATIKA UKUAJI WA SEKTA YA VIWANDA NA FURSA YA AJIRA
NA
MWANDIHI MAALUM
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde
ameishukuru sekta binafsi kwa mchango mkubwa inaoutoa katika sekta ya Uchumi wa
Viwanda na fursa za Ajira inazozitengeneza kupitia uwekezaji.
Naibu
Waziri Mavunde ameyasema hayo katika uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji
kikali cha K-VANT katika Hotel ya Serena Jijini Dar es salaam ambapo pia
amechukua fursa hiyo kuipongeza kampuni ya MEGA BEVERAGES kwa kutoa fursa za
AJIRA kwa wananchi zaidi ya 1000 na pia kwa uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha
vinywaji na kuitaka kampuni hiyo kuzingatia ubora ili kuifanya bidhaa yao kuwa
shindani na kuvuka mipaka ya Tanzania.
Akimkaribisha
Mgeni Rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni MEGA BEVERAGES Bw. Francis Kimaro
ameishukuru Serikali kwa mazingira wezeshi yaliyofanikisha uwekezaji huo wa
kiwanda na kuahidi kuzalisha bidhaa zenye ubora.
MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI JIJINI DODOMA LEO TAREHE 31 AGOSTI 2018.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri , kushoto ni Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, kikao hicho
kimefanyika kwenye ukumbi wa TAMISEMI, Mkapa House leo jijini Dodoma.
Kikao kikiendelea
Kikao kikiendelea
Naibu
Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza
la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
16 WANAODAIWA KUKWAPUA FEDHA ZA USHIRIKA WILAYANI HAI ,WAWEKWA NDANI KWA AMRI YA DC SABAYA
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
akizungumza wakati wa mkutano wa utoaji wa taarifa ya uchunguzi wa
kamati iliyoundwa na mkuu huyo kuchunguza ubadhilifu wa fedha za
Ushirika wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
akiwahoji baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Mijongweni
kuhusiana na ubadhilifu uliofanyika katika Ushirika huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
,akizungumza juu ya maamuzi yaliyochukuliwa mara baada ya kamati
aliyoiunda kuwasilisha taarifa yake.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na Mkuu huyo wa wilaya .
Baadhi ya wananchi wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wera akizungumza katika mkutano huo.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mijongweni ,Omary Mohamed akizungumza kwa niaba ya wananchi wengine katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
akitizama baadhi ya mashine zilizotolewa kwa Ushirika huo ambazo
zinatajwa kutumika huku mapato yake hayajulikani yalipo.
Moja ya Mashine hizo ikiwa tayari imeharibika baada ya kuondolewa Roller inayotumika kwa ajili ya kutembelea.
Mashine mpya ya Ushirika huo ambayo haijaanza kutumika bado.
Baadhi ya watuhumiwa wa ubadhilifu wa
fedha za Mradi wa Ushirika huo wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada
ya kukamatwa wakiwa eneo la mkutano.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
-WADAIWA KUFANYA UBADHILIFU WA ZAIDI YA MIL 200.
-WENGINE WAUZA VIPURI VYA MASHINE.
WATU
16 wakiwemo viongozi wa Bodi ya Ushirika wa Umoja wa watumia maji
katika kijiji cha Mijongweni (UWAMI) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya wakituhumiwa
kuhusika na ubadhilifu wa fedha za mradi zaidi ya
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)