Friday, August 31, 2018

TAASISI YA MOYO YAANZISHA KITENGO CHA HUDUMA KWA MTEJA (CUSTOMER CARE)


Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Taasisi hiyo Agnes Kuhenga
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (kushoto) akitoa maelekezo ya namna ya kutoa huduma bora kwa waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Idara ya Uuguzi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya (kulia) akitoa mada ya namna ya kupokea wagonjwa kwa waajiriwa wa kampuni ya Professional Cleaner watakaokuwa wanatoa huduma kwa mteja (customer care) kwa wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.


Mfanyakazi wa kampuni ya Professional Cleaner ambaye ni mmoja kati ya watoa huduma kwa mteja (customer care) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Khadija Abeid akielezea namna ambavyo atakua akitoa huduma bora kwa wateja wakati wa mafunzo mafupi ya utoaji wa huduma bora kwa mteja leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam.(Picha na: Genofeva Matemu)

No comments :

Post a Comment