Friday, August 31, 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA SEKTA BINAFSI KWA MCHANGO MKUBWA KATIKA UKUAJI WA SEKTA YA VIWANDA NA FURSA YA AJIRA

  NA MWANDIHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ameishukuru sekta binafsi kwa mchango mkubwa inaoutoa katika sekta ya Uchumi wa Viwanda na fursa za Ajira inazozitengeneza kupitia uwekezaji.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo katika uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji kikali cha K-VANT katika Hotel ya Serena Jijini Dar es salaam ambapo pia amechukua fursa hiyo kuipongeza kampuni ya MEGA BEVERAGES kwa kutoa fursa za AJIRA kwa wananchi zaidi ya 1000 na pia kwa uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji na kuitaka kampuni hiyo kuzingatia ubora ili kuifanya bidhaa yao kuwa shindani na kuvuka mipaka ya Tanzania.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni MEGA BEVERAGES Bw. Francis Kimaro ameishukuru Serikali kwa mazingira wezeshi yaliyofanikisha uwekezaji huo wa kiwanda na kuahidi kuzalisha bidhaa zenye ubora.






No comments :

Post a Comment