Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
akizungumza wakati wa mkutano wa utoaji wa taarifa ya uchunguzi wa
kamati iliyoundwa na mkuu huyo kuchunguza ubadhilifu wa fedha za
Ushirika wa watumia maji katika kijiji cha Mijongweni.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
akiwahoji baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Mijongweni
kuhusiana na ubadhilifu uliofanyika katika Ushirika huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
,akizungumza juu ya maamuzi yaliyochukuliwa mara baada ya kamati
aliyoiunda kuwasilisha taarifa yake.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini juu ya maamuzi yaliyochukuliwa na Mkuu huyo wa wilaya .
Baadhi ya wananchi wakionesha mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano huo.
Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wera akizungumza katika mkutano huo.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mijongweni ,Omary Mohamed akizungumza kwa niaba ya wananchi wengine katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya
akitizama baadhi ya mashine zilizotolewa kwa Ushirika huo ambazo
zinatajwa kutumika huku mapato yake hayajulikani yalipo.
Moja ya Mashine hizo ikiwa tayari imeharibika baada ya kuondolewa Roller inayotumika kwa ajili ya kutembelea.
Mashine mpya ya Ushirika huo ambayo haijaanza kutumika bado.
Baadhi ya watuhumiwa wa ubadhilifu wa
fedha za Mradi wa Ushirika huo wakiwa kwenye gari la Polisi mara baada
ya kukamatwa wakiwa eneo la mkutano.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
-WADAIWA KUFANYA UBADHILIFU WA ZAIDI YA MIL 200.
-WENGINE WAUZA VIPURI VYA MASHINE.
WATU
16 wakiwemo viongozi wa Bodi ya Ushirika wa Umoja wa watumia maji
katika kijiji cha Mijongweni (UWAMI) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya wakituhumiwa
kuhusika na ubadhilifu wa fedha za mradi zaidi ya Sh Mil 200.
Mbali
na Viongozi wa Bodi ya ushirika huo wakiongozwa na Mwenyekiti wake
,Nuru Ndoma pia wamo baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji, Viongozi
wa kamati ya mpito ya kusimamia mradi huo ikiongozwa na Alex Mkwizu.
Kukamatwa
kwa Viongozi hao kunatokana na taarifa ya uchunguzi uliofanywa na
kamati iliyoundwa na Mkuu huyo wa wilaya kuchunguza madai ya ubadhilifu
wa fedha baada ya kukataa taarifa yaawali ya kamati kama hiyo
iliyoundwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Gelasius Byakanwa.
Tuhuma
zinazowakabili watu hao zimetajwa kuwa ni pamoja na kuuzwa kinyemela
kwa Mashine ya kulimia (Power tiller ) aina ya Kubota iliyotolewa na
Wizara ya Kilimo kwa kijiji cha Mijongweni ambayo inatajwa kuuzwa kwa
mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Yusuph Losindilo.
Baadhi
ya viongozi hao pia wanatajwa kutakatisha fedha za malipo ya
ukodishwaji wa mashine ya kuvunia Mpunga kwa kuziingiza katika akaunti
ya kijiji na kasha kuzitoa wakati huo huo na kuzipangia matumizi
yasiyokuwa na maelezo ya kutoshereza.
Aidha
watu hao pia wanadaiwa kuuza baadhi ya vipuri vya Mashine hizo na
baadae kuonesha kuwa wamenunua vipuri kwa ajili ya matengenezo ya
mashine hizo huku ikionyesha vipuri vinavyodaiwa kununuliwa ni vile
vilivyoletwa pamoja na mashine.
Katika
taarifa yake ,Mwenyekiti wa kamati hiyo maalumu ya uchunguzi ,Valeria
Banda alisema wizara ya Kilimo ,chakula na Ushirika kupitia Halmashauri
ya wilaya ya Hai ilipeleka mashine tano za kuvuna na moja ya kupura
mpinga kwa lengo la kupunguza adha ya wananchi kuvuna na kupura mpunga
kwa kutumia mikono.
“Lengo
jingine la kutolewa kwa mashine hizi ilikuwa ni kuongeza chanzo cha
mapato kwa wananchi wa kijiji cha Mijongweni ,mashine tatu zenye thamani
ya Sh Mil 222.5 zilikuwa ni Combine Harvester aina ya Kubota , mbili
aina ya Daedong na moja ya Kupura mpunga (Paddy thresher) zenye thamani
ya Sh Mil 152.8”alisema Valeria.
Alisema
katika kuendeleza ubadhilifu watu hao wanadaiwa kushindwa kusimamia
matumizi ya mashine hizo ambapo inadaiwa wajumbe wa bodi walipangiana
zamu ya kusimamia mashine izo wakati wa zoezi la uvunaji kwa maslahi yao
binafsi huku wengine wakivuna nyakati za usiku bila kuwasilisha hesabu
za mavuno hayo kwa uongozi.
“Mfano
Mayunga Mathayo anatuhumiwa kuvuna nyakati za usiku na kutowasilisha
hesabu za fedha alizokuwa anapata ,hali iliyosababisha afukuzwe kuwa
mjumbe wa bodi.Mayunga pia aliuza Hydrolic pump (Orignal) aina ya Kubota
yenye thamani ya sht Mil 5 ya mashine namba tisa ya kuvuna mpunga na
kufunga pump isiyo na ubora kwenye mashine hiyo ambayo kwa sasa
imeharibika.”alisema Valeria.
Valeria
alisema fedha zilizokuwa zinapatikana shambani zaidi ya asilimia 50
zilifanyiwa matumizi shambani na wakati mwingine fedha zote zilitumika
huko huko shambani bila kufikishwa ofisini na hata zilizofikishwa bado
zilipangiwa tena matumizi.
“Baada
ya fedha kufanyiwa matumizi zilizobaki zilipelekwa SACCOS ya jitegemee
na kutolew wakati huo huo kwa matumizi mengine yasiyo na kibali wala
vithibitisho vyovyote ,mfano Oktoba 18 ,2016 kiasi cha sh 810,000
ziliingizwa kwenye akaunti na tarehe hiyo hiyo Sh 800,000 zikatolewa
,katibu wa Bodi Severa Kimati aliyehusika kuziweka na kuzitoa hakuwa na
maelezo ya kutosha zaidi ya kusema alitumwa na mwenyekiti wa Bodi Nuru
Ndoma”alisema Valeria.
Alisema
fedha ambazo zingetakiwa kuwekwa katika akaunti ya kijiji toka
Machi,2016 wakati mashine hizo zikianza kufanya kazi hadi kufikia Juni
,2018 kipindi ambachowalifanya kazi wajumbe wawili kutoka kwenye jamii
zilipaswa kuwa Sh Mil 285.6 lakini kiasi kilichopo ni Sh Mil 10.9 ambazo
zilipatikana baada ya afisa mtendaji na afisa ugani kuamua kusimamia
mashine moja katika kipindi cha mwezi mmoja.
Akizungumza
baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo ,Mkuu wa wilaya ya Hai,Lenga Ole
Sabaya alimuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Hai,Lwelwe Mpina kumkamata
aliyekuwa Mkuu wa idara ya Ushirika wa wilaya hiyo , Raphael Mbwambo
ambaye alitajwa pia kuhusika katikaubadhirfu huo.
Alisema
viongozi wa Bodi, ya Ushirika huo hawakuwa na uhalali kutokana na
kwamba hakuna wanahisa wala wanachama waliokaa na kuwachagua na kwamba
waliteuana kwa maslahi yao binafsi huku akitaka fedha zote zilizopotea
kurejeshwa.
“HAwa
viongozi wa Bodi kwa kushirikiana na wajumbe wa serikali ya kijiji
warudishe fedha walizoiba za wananchi wanyonge wa kijiji cha Mijongweni
,Nimeelekeza wasiingie kwenye ofisi yoyote ya umma,hawa ni waharifu kama
waharifu wengine hadi itakapothibitika vinginevyo.”alisema Ole Sabaya.
Wanaoshikiliwa
ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo ,Nuru Ndomba na Katibu
wake wake Severa Kimati pamoja na wajumbe wengine, Salama
Amani,Sadiki Msangi, Abuu Musa na D eogratius Bruno,.
Wengine
ni Alex Mkwizu, Mashati Amani, Bakari Malola, Adamu Mdaki,Mayunga
Mathayo ,Abdalah Dhamiri,Richard Msele,Ramadhan Miraji ,Miraji Araba na
Koswai Mrisho.
No comments :
Post a Comment