Khatib Suleiman, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema
sheria ya kumlinda mwanafunzi aliyepata ujauzito kuendelea na masomo
itaendelea kufanya kazi kwa sababu imeleta matumaini makubwa kwa
wanafunzi wa kike.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wanawake na Watoto, Mouldine Castico amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya utetezi kwa taasisi zinazoshughulikia haki kwa watoto Zanzibar.
Amesema lengo la sheria hiyo ni kuwawezesha wanafunzi wa kike kuendelea na masomo na mimba si kumfanya maisha yake yakwame.
Alisema yapo mafanikio wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo wengine wakifaulu kwenda kidatu cha nne na sita.
''Zanzibar tuna sheria ya mwanafunzi anayepata ujauzito kuendelea na masomo ambayo lengo lake ni kumwezesha mtoto wa kike asipate kikwazo kupata elimu ya msingi,'' amesema.
Alisema serikali itatunga sheria za maslahi ya mtoto wa kike kuondoa vikwazo vinavyofanya watoto hao washindwe kuendelea na masomo.
Mfano, alisema SMZ imeimarisha haki za watoto katika magereza pamoja na vyombo vya sheria mahakamani kupata haki zao haraka.
Amesema, mahakama za watoto zimeimarishwa ambapo kwa sasa hakuna mtoto chini ya miaka 18 anayefikishwa katika mahakama za kawaida.
''Tumepiga hatua kubwa kuimarisha haki za watoto ambapo sasa tuna mahakama za watoto zinazofanya kazi zake vizuri,'' alisema.

No comments :
Post a Comment