Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt.
Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika Mkutano ulioandaliwa na Bohari ya
Dawa (MSD), uliowakutanisha na wazalishaji wa dawa na vifaa tiba kutoka
ndani na nje ya nchi uliofanyika leo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ambapo wazalishaji zaidi
ya
130 kutoka nchi 25 walihudhuria.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu akizungumza.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante ole Gabriel, akizungumza katika mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa MSD wakifuatilia mkutano huo.
Wafanyakazi wa MSD wakiwa katika mkutano huo.
Wazalishaji dawa na vifaa tiba wakiwa kwenye mkutano.
Wafanyakazi wa MSD, wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mwakilishi wa Wazalishaji wa ndani, kutoka Kiwanda cha Prince Phermaceutical,Hetal Vitalan, akizungumza.
Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Abdul Mwanja akizungumza.
Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Adonis Bitegeko, akizungumza.
Wazalishaji dawa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Na Dotto Mwaibale
KATIBU
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,
Dkt.Mpoki Ulisubisya, amesema uwezo wa Bohari ya Dawa (MSD), umeongeza
na kupanua wigo wa uwekazaji na uzalishaji wa dawa nchini.
Akizungumza
kwenye Mkutano wa pili wa mwaka wa MSD na wazalishaji na washitiri wa
dawa na vifaa tiba zaidi ya 130 kutoka nchi 25, Dkt. Mpoki amesisitiza
kuwa, MSD niya kiwango cha kimataifa hivyo milango iko wazi kwa
wawekezaji wa dawa na vifaa tiba kuja kuwekeza nchini.
Aliongeza
kuwa mkutano huo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na kujadili namna
yakufanya manunuzi,utekelezaji wamikataba na uimarishaji wa uwekezaji
katika sekta ya afya.
“Tunaitikia
wito wa serikali wa kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanapewa
kipaumbele, hivyo mkutano huu wakiutendaji,utaijengea uwezo MSD na
kuongeza ushirikiano kati yake na wawekezaji wa viwanda vya dawa na
vifaa tiba kwa kujua mahitaji aliyopo na kuwashauri soko tulilonalo
ndani na njeya nchi ilikupanua wigo wautendaji,”alisema.
Aidha
alisisitiza kuwa uwezo wa MSD katika usambazaji wa dawa na vifaa tiba
umekua na ndio sababu ya kukidhi viwango vya kimataifa, huku mwaka wa
fedha uliopita wakiwa wameweza kutumia dola milioni 700 kwa ajili ya
kufanya manunuzi.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.
Elisante Ole Gabriel, alisema utendaji wa MSD meboresha huduma za afya
nchini na uhusiano wa karibu kati ya wizara yake na sekta ya afya
nikichocheo muhimu cha uchumi nchini.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu, alisema hatua ya
bohari kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, imewawezesha
kupanua wigo wa huduma na kuwa karibu na wafanyabiashara na wawekezaji
160 alioingia nao mikataba, hivyo mkutano huo utawajengea uwezo na
kuongeza ushindani kwa wazalishajihao.
Aidha,
kwa upande wake mwakilishi wa wazalishaji wa ndani, kutoka kiwanda cha
Prince Phermaceutical,HetalVitalan, lisema uimarishaji wa viwanda vya
dawa na vifaa tiba hapa nchini,umesaidia fedha inayotengwa na serikali
katika bajeti ya dawa kuweza kukuza uchumi wa ndani,kuongeza ajira kwa
watanzania na kupanua wigo waukusanyaji wa kodi kwa viwanda vya ndani.
No comments :
Post a Comment