Tuesday, July 17, 2018

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI NA STL GROUP


 Balozi Seif akimsisitiza jambo Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Amand Group iliyo chini ya Taasisi ya STL Group  Bwana Nadas Simhoni aliyeuongozi ujumbe wa viongozi wanne wa Kampuni hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
(katikati), akizungumza na uongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kitaalamu inayosimamia Makampuni  Sita yanayojihusisha na masuala ya Miundombinu, Afya, Elimu, Biashara, Umeme na Mawasiliano ya Kisasa ya STL Group huko Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

NA OMPR, ZANZIBAR
UONGOZI wa Taasisi ya Kimataifa ya Kitaalamu inayosimamia makampuni  sita yanayojihusisha na masuala ya Miundombinu, Afya, Elimu, Biashara, Umeme na Mawasiliano ya Kisasa-STL Group imeonyesha nia ya kutaka kuiunga mkono Zanzibar ili iweze kuongeza nguvu za uwezeshaji katika kubuni mbinu na
maarifa kwenye Sekta tofauti. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Amand Group iliyo chini ya Taasisi hiyo Bw. Nadas Simhoni aliyeuongoza ujumbe wa viongozi wanne wa Kampuni hiyo alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bw. Simhoni alisema Amand Group yenye wataalamu wa kutosha ambao tayari wanawajibika katika mataifa ya Ghana, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Togo, Ivory Coast na Tanzania wana uzoefu mkubwa wa kusarifu mambo tofauti ikiwemo michoro ya majengo mbalimbali.Alisema miradi ya maendeleo ya sekta za Elimu,
Afya na Kilimo ambazo huijumuisha Jamii  ndiyo vipaumbele
vikubwa walivyoviangalia zaidi ambavyo utekelezaji wake hujumuisha jamii katika ngazi ya Kitaifa na Jumuiya za Kijamii.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi aliuhakikishia uongozi wa taasisi hiyo ya STL Group kwamba  Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar  iko tayari  kuipatia ushirikiano taasisi hiyo katika
azma yake ya kuunga mkono maendeleo ya Zanzibar.

Hata hivyo Balozi Seif  aliuambia uongozi wa taasisi hiyo kwamba  serikali
imeweka utaratibu maalum wa kutoa tenda pale inapotaka kuanzisha miradi
yake ya kiuchumi na ya kijamii jambo ambalo uongozi huo una fursa ya
kuomba tenda hizo zinapotokea.

Taasisi ya kimataifa ya kitaalamu  ya STL Group inasimamia Makampuni  Sita
yanayojihusisha na masuala ya Miundombinu ya Ujenzi, Sekta za Afya, Elimu,
Biashara, umeme, Mafuta, Gesi pamoja na Mtandao wa Mawasiliano ya Kisasa .
Makampuni hayo ni pamoja na Super Tech Limited, Amand Energy, Amand, Agritop Limited, Super Lock pamoja na SAF STL Amand.

No comments :

Post a Comment