Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Bw. Faustine Mdesa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna wa Kodi za Ndani Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo (kushoto)
akimwelezea jambo Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na watendaji wengine wa TRA
aliofuatana nao kuhusu namna sekta ya utalii nchini inavyochangia pato
kubwa kwa Serikali wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna huyo Jijini
Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya
utalii nchini.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA)
………………………………..
Na Rachel Mkundai, Arusha
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha
kwamba
pato la Serikali na kodi stahiki inapatikana kupitia sekta ya
utalii nchini.
Akizungumza
Jijini Arusha, Kamishna wa Kodi za Ndani, Bwana ELIJAH
MWANDUMBYAamesema kwamba, sekta ya utalii ni moja ya sekta inayoiingizia
Serikali fedha nyingi za kigeni na hivyo inahitaji mkakati madhubuti
ili kuongeza pato kwa Serikali
“Sekta
ya utalii inaingizia serikali fedha nyingi za kigeni, TRA tumekuja na
mkakati maalum ili kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia pato la taifa
kupitia kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi”, amesema Kamishna wa
kodi za ndani.
Mwandumbya
ameongeza kuwa kwa muda mrefu sekta ya utalii imekuwa ikifanya vizuri
lakini bado inahitaji mkakati wa kuhakikisha kwamba kila pato
linaloingia kupitia sekta hii linaongeza tija kwenye mapato ya nchi
kupitia kodi mbalimbali kama zilivyoainishwa na sheria za kodi.
Aidha,
Kamishna Mwandumbya amefafanua kuwa moja ya mikakati hiyo ni
kushirikiana na taasisi zingine za serikali zilizopo kwenye sekta ya
utalii zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro na Chama cha wafanyabiashara wa Utalii (TATO)
pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wanaojihusisha
na utalii.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Bwana
Allan Kijazi amesema TANAPA ipo tayari kushirikiana na TRA pamoja na
taasisi zingine za serikali kwa kuwa lengo ni kukusanya mapato ya
serikali na hivyo kuhakikisha kuwa mapato yanayopatikana kupitia utalii
yatanufaisha nchi kwa kuleta tija katika mapato.
“Sisi
sote ni taasisi za serikali , tunajenga nyumba moja, tutashirikiana
nanyi ili serikali yetu Isimame imara na kupata kodi stahiki”, amesema
Bw Kijazi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO),
Bwana Wilberd Chambulo amewataka Wafanyabiashara wanaojihusisha na
masuala ya utalii kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa manufaa ya nchi
ambapo pia ameunga mkono ujio wa mkakati huo maalum wa TRA wa kuongeza
mapato kupitia sekta ya utalii.
Sekta
ya utalii inatajwa kuwa moja ya sekta inayoiingizia Serikali fedha za
kigeni hata hivyo takwimu zinaonesha kuwa kuna wafanyabiashara 2,200
wanaotambulika katika utalii nchini na kati ya hao 1,403 wanafanya
shughuli zao katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga
Hivyo,
utekelezwaji wa mkakati huo utaipelekea Serikali kuongeza makusanyo ya
mapato yake na kukuza maendeleo kwa wananchi katika kutoa huduma
mbalimbali za kijamii.
No comments :
Post a Comment