Wananchi wa Kata ya Kumbulu,
Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge – Miundombinu, Mhe mbunge Rashid Mohammed
Chwachwa (Masasi- aliyejifunga shuka) wakati wa uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu
kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu,
Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Naibu
Waziri wa Miundombinu – Mhe Eng Atashasta Ndikiye (katikati aliyevaa
kofia) wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo
unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika
kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu,
Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakiigiza adha walizokuwa wanazipata
kupata mawasiliano ya uhakika ya simu wakati wa uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu
kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo. Mnara huo pamoja na
mingine katika kata za Balama na Nongwe ilijengwa kwa ushirikiano baina
ya Tigo na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuzinduliwa na
wahemshimiwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano ya Bunge.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Kakoso (wa tatu kulia),
akishirikiana na Naibu Waziiri wa Miundombinu, Mhe Eng Atashasta Ndikiye
(katikati aliyevaa kofia), Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya
Miundombinu, viongozi wa serikali, pamoja na wakurugenzi wa
kampuni ya simu ya Tigo na Mfuko wa Kudumu wa Mawasiliano kwa Wote
(UCSAF) kukata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa mawasiliano
uliojengwa na UCSAF na Tigo ili kuwezesha mawasiliano ya simu kwa mara
ya kwanza katika kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro juzi.
…………………..
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mawasiliano pamoja na Naibu Waziri wa Miundombinu Washiriki Kuzindua
Minara Mipya Katika Kata za Kumbulu and Balama,Wilaya ya Gairo
Gairo, Julai 18, 2018; Ikiwa
sehemu ya juhudi zake kuhakikisha kuwa kila mtu anashiriki kukuza uchumi
wan chi na kupata maendeleo yatokanayo na huduma bora za mawasiliano,
kampuni ya Tigo Tanzania imepanua mtandao wake katika maeneo ya
pembezoni katika kata za Kumbulu and Balama yaliyopo wilaya ya Gairo,
Mkoani Morogoro.
Akizindua minara hiyo mipya
inayowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza kabisa
katika kata hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu. Mheshimiwa Seleman Kakoso alisema kuwa upatikanaji wa
huduma za mawasiliano huleta mabadiliko makubwa ya ukuaji wa uchumi,
ubunifu na maisha ya watu kwa ujumla. Mhe Kakoso alimbatana na Naibu
Waziri wa Miundombinu, Mhe Eng. Atashasta Ndikiye, waheshimiwa wabunge
ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu pamoja na
viongozi wengine wa serikali.
‘Nawashukuru Tigo kwa kuitikia
mwito wa Serikali na kushiriki kikamilifu katika kuunganisha maeneo haya
ya pembezoni ambayo hapo zamani hayakuwa na mawasiliano yoyote ya simu
kwa sababu hayana mvuto mkubwa wa kibiashara. Ninatoa wito kwa kampuni
nyingine za simu kuiga mfano huu ili kuhakikisha kuwa kila mtu anapata
fursa ya kuwa sehemu ya mageuzi makubwa yatokanayo na Tehama, huku
wakizingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali katika kutimiza
miradi ya aina hii,’ alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Dk Joseph Kilongola alibainisha kuwa
minara hiyo ilikuwa imejengwa kwa ushirikiano baina ya UCSAF na Tigo
kama sehemu ya zabuni ya zinazolenga kuunga mkono juhudi za Serikali za
kuhakikisha mawasiliano ya uhakika kwa wananchi wote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Tigo, Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa alisema kuwa lengo kuu la Tigo
ni kuwaunganisha Watanzania zaidi ya milioni 13 ambao kufikia sasa bado
hawana huduma za mawasiliano.
‘Tigo inaamini kuwa
upatikanaji wa mawasiliano utaibua fursa mpya za kiuchumi, elimu, afya,
biashara na kubadili maisha ya watu,’ alisema.
Mutalemwa alisema kuwa kampuni ya
Tigo imelenga kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga Tanzania ya
viwanda kwa kupanua mtandao wake ili kuwezesha nchi nzima kufurahia
faida za utandawazi utakanao na mawasiliano ya uhakika.
“Tunafuhari kuwa Serikali
imetambua tofauti kubwa ya upatikanaji wa mawasilaino iliyopo baina ya
maeneoa ya mijini na vijijini, na kujitolea kwake kufadhili zabuni mbali
mbali zinazowezesha kampuni za simu kufikisha huduma za mawasiliano
katika maeneo mbali mbali kama kata hizi za Balama, Kumbulu na Nongwe
ambazo hapo awali hazikuwa na huduma yoyote ya mawasiliano ya simu kwa
sababu hazina mvuto mkubwa wa biashara,’ alisema.
Tigo imeshiriki katika zabuni
za UCSAF tangu mwaka 2012 ambapo kufikia sasa imefanikiwa kushinda
zabuni zilizoiwezesha kuunganisha zaidi ya kata 100 na huduma za
mawasiliano.
No comments :
Post a Comment