Wachezaji
wa timu ya TBL Group FC ambao ni mabingwa wa kombe la Standard
Chartered 2018 wakiwasili makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini Dar
es Salaam wakati wa hafla ya kupongezwa
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani
(Kushoto) akiwa na maofisa wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi wa TBL
Group Ilala jijini Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi
Mkuu wa wa TBL Group na Rais wa kitengo cha ukuzaji wa Masoko wa ABinBev
kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin,wakati wa mkutano wa kupongeza
wachezaji wa TBL FC
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (Kushoto) akifafanua jambo katika mkutano huo
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered , Juanita Mramba,akitoa maelezo kuhusiana na ziara hiyo
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group na Rais wa kitengo cha ukuzaji wa Masoko wa ABinBev
kanda ya Afrika Mashariki, Roberto Jorrin ( kushoto) akiwa na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa
pili kulia ) pamoja na wachezaji wa timu ya TBL FC wakishangilia kombe
wakati wa hafla ya kuipongeza
Wafanyakazi wa TBL na Standard Chartered katika picha ya pamoja katika hafla ya kuipongeza TBL FC
………………….
TBL FC Kwenda Uingereza kutembelea klabu ya Liverpool
-Kushuhudia mechi ya ligi ya Uingereza Live
Bingwa
wa mashindano ya soka ya makampuni yaliyoandaliwa na Benki ya Standard
Chartered,
mapema mwezi uliopita,TBL FC, itaondoka nchini mwezi septemba
2018 kwenda nchini Uingereza, kutembelea klabu maarufu ya Liverpool
pamoja na kukutana na wachezaji mashuhuri wanaochezea klabu hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered,
Sanjay Rughani,wakati alipofanya ziara makao makuu ya TBL Group Ilala
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipongeza timu hiyo sambamba na
kukutana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo.Alibainisha kuwa watakuwa
nchini Uingereza kati ya Novemba 8 na Novemba 10 ambapo pia watashuhudia
mechi ya mchezo wa ligi kuu ya Uingereza , kati ya timu ya Fullham na
Liverpool utakaopigwa katika uwanja wa Anfield.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TBL Group,Roberto Jarrin, aliipongeza benki ya Standard
Chartered, nchini kwa ubunifu mkubwa wa kuwaunganisha wateja wake
kupitia Nyanja ya michezo sambamba na utoaji huduma bora kwa wateja
wake.
Mashindano
ya Standard Chartered 2018 yalifanyika mwezi uliopita na kushirikisha
timu za makampuni mbalimbali ambao ni wateja wa benki hiyo na kufanyika
katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Saalaam ambapo TBL FC, iliibuka
na ushindi wa kuifunga timu ya kampuni ya Mwananchi Communication mabao
3-2 kwa njia ya penalti na kujihakikishia ubingwa wa michuano hiyo.
Nahodha
wa timu hiyo,Lupa Mwanjopa,alitoa shukrani kwa mwandaaji wa mashindano
hayo na kueleza kuwa wamefurahi kupata fursa hiyo ya kwenda nchini
Uingereza sambamba na kutembelea klabu ya Liverpool na kukutana na
wachezaji nguli wa timu hiyo “Michezo ni moja ya jukwaa la
kuwaunganisha watu pamoja na kujenga afya,tunashukuru Benki ya Standard
Chartered kwa kuipa umuhimu na kuwajali wateja wake”alisema.
Mkuu
wa Uhusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba, alisema kuwa mbali
na kutembelea klabu hiyo pia watapata nafasi ya kufanya mazoezi katika
akademi ya klabu hiyo katika uwanja wa Anfield pamoja na kutembelea
maeneo mbalimbali ya uwanja huo kabla ya kwenda kuangalia mchezo wa
wapinzani wa Liverpool.
No comments :
Post a Comment