Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (kulia) akibadilishana mawazo na wadau wa maendeleo
mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa
Mataifa kabla ya kuanza kwa mkutano wa kamati ya maandalizi ya
utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika
jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga na Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa Kigoma, Evance Siangicha (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kamati ya
maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP)
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa
jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa kamati
ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma
(KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia
Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma, Charles Pallangyo.
Picha ya pamoja ya washiriki
wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja
ya kusaidia Kigoma (KJP) wakiwemo wadau wa maendeleo uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mchambuzi Mratibu wa Umoja
wa Mataifa (UN Coordination Analyst )nchini, Kanali Rankho akitoa
maelekezo kwa Adrian Fitzgerald kutoka Irish AID wakati washiriki wa
mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya
kusaidia Kigoma (KJP)walipokuwa wakiwasili katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Kansela wa Ubalozi wa Norway,
Britt Kjolas akitoa salamu kwa niaba ya wadau wa maendeleo wakati wa
mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya
kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma, Charles Pallangyo (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa
kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia
Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa
Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,
Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (wa pili kulia)akizungumza
wakati akifungua mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa
programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Wengine
katika picha ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo
(kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto)
pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula
Duniani (WFP) nchini, Michael Dunford (kushoto).
Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa Kigoma, Evance Siangicha akiwasilisha rasimu ya makubaliano ya
utekelezaji wa Programu ya KJP wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi
ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP)
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa
jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mchambuzi Mratibu wa Umoja wa
Mataifa (UN Coordination Analyst )nchini, Kanali Rankho
Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa Kigoma, Evance Siangicha akifafanua jambo wakati akiwasilisha
hatua iliyofikiwa kwenye programu nzima ya KJP wakati wa mkutano wa
kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia
Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa
Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Prisca
Mgomberi akiwasilisha hatua iliyofikiwa katika uwezeshaji kiuchumi kwa
wanawake na vijana wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya
utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es
Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini, Viola Kuhaisa akiwasilisha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji
wa eneo la elimu wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya
utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es
Salaam.
Mwakilishi kutoka Shirika la
Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) nchini, Stephanie
Shanler akiwasilisha hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi wa
KJP eneo la kuzuia ukatili kwa wanawake na watoto wakati wa mkutano wa
kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia
Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa
Mataifa jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni
washiriki wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu
ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Shirika la Umoja
wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini, Kajsa Nyerere
akiwasilisha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa program ya KJP
katika eneo la kilimo wakati wa mkutano wa kamati ya maandalizi ya
utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia Kigoma (KJP) uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es
Salaam.
…………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
MKUU wa mkoa wa Kigoma
Emmanuel Maganga amesema serikali ya Tanzania inafurahishwa na namna
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyofanya kila linalowezekana kusaidia
kuboresha
maisha ya wananchi wa mkoa wa Kigoma ambao ndio wenyeji wa
wenzao wanaokimbia matatizo nchi jirani.
Akizungumza katika mkutano wa
kamati ya maandalizi ya utekelezaji wa programu ya pamoja ya kusaidia
Kigoma (KJP), alisema kazi kubwa inayofanywa na mashirika hayo ikiwamo
ya kupeleka ushawishi kwa wadau wa maendeleo ya kusaidia wananchi wa
Kigoma wakiwemo wageni wakazi na wakimbizi.
Akiwa Mwenyekiti mwenza wa
kamati hiyo, Maganga alisema pamoja na juhudi hizo bado mkoa una
changamoto nyingi zinazotakiwa kushughulikiwa japo serikali imeendelea
na juhudi za kuboresha mazingira ya miundombinu ya kuwezesha shughuli za
kiuchumi.
Alisema toka mkutano wa
mwisho mwaka jana, kumekuwa na maendeleo makubwa katika kampeni za
serikali za kuufungua mkoa huo kiuchumi kwa kutengeneza miundombinu
mbalimbali kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara.
Alisema serikali inaendeleza
miradi ya kimkakati hasa ya barabara zinazounga mkoa huo na nchi za
Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) na mikoa mingine
ya Tanzania ya Shinyanga, Mwanza, Kagera na Tabora.
Alisema mathalani kwa
kujengwa kwa barabara ya Nyakanazi – Kigoma kwa kiwango cha lami
kutafungua fursa za kiuchumi za mkoa huo. Aidha alisema kwamba
kumekuwepo na maboresho katika usafiri wa anga ambapo kwa sasa kuna
safari sita za ndege kwa wiki.
Akizungumzia kuhusu
umuhimu wa ushiriki wa wadau wote katika programu hiyo, alisema baada ya
mkutano wa Aprili 27 mwaka huu anaona kuwiwa sana na Umoja wa Mataifa
katika kuhakikisha kwamba kila mdau anashiriki kuhakikisha utekelezaji
wake.
Aliuomba Umoja wa Mataifa
kuwapatia elimu wabunge ambao walikosekana katika mkutano huo wa
kueleweshana kuhusu programu ili waweze kushiriki kikamilifu.Pia aliomba
Umoja wa Mataifa kufanyia kazi hoja ya kutanuliwa kwa programu hiyo
kufika katika wilaya zote za mkoa huo.
Mkuu huyo wa mkoa pamoja na
kumshukuru binafsi Mratibu wa mashirikia ya Umoja wa Mataifa nchini
Alvaro Rodriguez na Umoja wa Mataifa alisema kwamba kutokana na umuhimu
wa programu hiyo yeye binafsi atakuwa anaifuatilia na kuwataka watendaji
katika mkoa kuhakikisha kwamba wanatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa
programu yenyewe.
Naye Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez Alvaro Rodriguez akizungumza katika
kikao hicho alisema mradi wa utekelezaji wa pamoja wa Kigoma (KJP) ni
ajenda muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Umoja
wa Mataifa nchini Tanzania UNDAP II, wenye lengo la kutoa msaada wa
maendeleo kwa Tanzania ndani ya mpango wa maendeleo wa Tanzania wa miaka
mitano.
Alisema mpango huo umelenga
kuangalia changamoto za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mkoa wa
Kigoma na hivyo kuwezesha maendeleo endelevu (SDGs) kuweza kufanikiwa.
Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuhifadhi wakimbizi kutoka Burundi, Rwanda
na Kongo
Katika hotuba yake kwenye
kikao hicho alishukuru mataifa ya Sweden, Norway na Korea Kusini kwa
kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha programu hiyo ya maendeleo.
Mkuu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa pia alishukuru serikali ya
Tanzania kwa kuteua mtu ambaye atakuwa anashughulika na mradi huo moja
kwa moja. Aidha alishukuru wadau wengine wa mradi kwa kuliona hilo na
wao kuteua watu mahususi ambao wataangalia utekelezaji wa miradi katika
nafasi yao.
Mradi huo wa KJP unajumuisha
shughuli za kitaifa zenye lengo la kuwa kwamua wananchi wa Kigoma na pia
kuwawezesha kuhimili muingiliano wa tamaduni zingine kutokana na
kupokea wakimbizi. Mambo yanayofanyika katika mradi huo ni kukabili
ukatili wa kijinsia kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Kigoma, Uendelezaji
wa sekta ya kilimo (ASDP 2) na mradi wa maendeleo ya maji (WSDP).
Imeelezwa kuwa kufanikishwa
kwa mambo hayo kutawezesha mkoa huo kusonga mbele na kukamilisha malengo
ya maendeleo endelevu ya dunia.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa
katika mradi huo yenyewe yanatoa utaalamu wa kiufundi, fedha na msaada
wa kitaasisi kuhakikisha kwamba kazi zilizokusudiwa katika mradi
zinafanyika kwa kiwango kikubwa.
Alisema katika awamu ya
kwanza ya utekelezaji wa mradi huo wanawake na vijana wamejitwalia
nafasi ya kujifunza na pia kuwezeshwa katika elimu na kilimo.Kukamilika
kwa kituo cha mafunzo kumewezesha vijana 270 kila mwaka kupata elimu ya
ufundi kama tehama, useremala, utengenezaji wa sabuni na kadhalika hali
ambayo inatarajiwa kusababisha mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Pia mradi unashiriki katika
ujenzi wa masoko yasiyo na mpaka katika maeneo ya Kakonko na Kibondo na
kuanzishwa kwa makundi 61 ya uwekaji akiba yaliyo na wanachama 1400.
Aidha watoto 513 waliokuwa
wanaoishi katika mazingira magumu huku wakiwa wamefanyiwa ukatili wa
kijinsia wamepatiwa nyenzo muhimu za kusoma na wengine 3,900
walitambuliwa ujuzi wao na kwamba mipango iko mbioni kuhakikisha kwamba
wanashiriki katika uzalishaji mali.
Naye Kansela wa Ubalozi wa
Norway nchini Britt Kjolas amesema kwamba amefurahishwa shughuli
zinazoendelea katika mradi huo wa pamoja kuahidi nchi yake kuendelea
kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania
kuwezesha mabadiliko chanya katika mkoa wa Kigoma.
Alielezea kufurahishwa kwake
na kujitokeza kwa wingi kwa wadau wa mradi na kusema mradi huo upo
katika msingi mzuri wa mafanikio.
No comments :
Post a Comment