NA RS -TABORA
18 JULAI 2018
SERIKALI
inatarajia kutatoa shilingi milioni 300 kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Tabora (Kitete) kwa ajili kukamilisha chumba cha upasuaji na
uboreshaji wa maeneo mengine.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipotembelea Hospitali hiyo kwa ajili ya kujionea hali ya utoaji wa
huduma za afya mkoani humo.
Alisema
sehemu ya fedha itasaidia kuhakikisha inapanua chumba cha wazazi na
wodi ya upasuaji kwa ajili ya kuboresha zaidi hizo hizo Hospitalini
hapo.
Waziri
huyo alisema watahakikisha wanapeleka fedha hizo kabla ya Mwezi Desemba
mwaka huu ili kuhakikisha mwanamke anapojifungua anakuwa salama yeye na
mtoto wake.
Aidha,aliwaagiza
viongozi wa hospitali hiyo kuwa wabunifu kwa kununua vifaa vyote muhimu
vinavyowezekana kuliko kusubiri Wizara kuwaletea kwa ajili ya
kuhakikisha huduma muhimu zinakuwepo na wananchi wanapata matibabu kwa
gharama nafuu.
Hata
hivyo aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na
miiko ya utumishi wa umma ili kuondoka malalamiko kwa wananchi wanaofika
kupata huduma katika hospitali hiy.
Alisema
uongozi wa Hospitali hiyo usimuone haya mtumishi ambaye ataonyesha
vitendo vya ubaguzi na utoaji wa lugha chafu kwa wagonjwa wakati wa
kutoa huduma.
Naye
Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Munde Tambwe aliupongeza Uongozi wa
Hospitali ya Kitete kwa kuboresha hali ya usafi katika wodi mbalimbali
na kusema hivyo mazingira ya wodini ni mazuri hakuna harufu kama siku za
nyumba.
Alimuomba
Waziri huyo mwenye dhamana na masuala ya afya kuwaongezea watumishi
kutokana na kuzidiwa na wagonjwa , hali inayowafanya wananchi kuchelewa
kupata huduma ya matatibabu.
Munde alisema hali hiyo ndio imepelekea baadhi ya wagonjwa kulalamikia kuwa kuna huduma mbaya kumbe watumishi wamezidiwa.
No comments :
Post a Comment