Kushoto ni Mkurugenzi wa Redio Habari Maalumu, akijitetea mbele ya viongozi wa TAMUFO.
Viongozi
wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Kwaya mbalimbali na Uongozi
wa Redio Habari Maalumu wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya
matumizi ya kazi zao. Kulia ni Rais wa TAMUFO, Dk.Kisanga na nyuma yake
ni Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel.
Mwenyekiti wa Kwaya za Ulyankulu aliyeshika faili akieleza jinsi nyimbo zao zinavyotumika mitandaoni pasipo kunufaika nazo.
Picha ya
pamoja baada ya mkutano huo. Wa tatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa
TAMUFO, Stellah Joel na wa pili ni Mkurugenzi wa Redio Habari Maalumu.
Viongozi
wa TAMUFO, Dk.Donald Kisanga na Katibu wake, Stellah Joel, studio ya
Arusha One Redio kuhakikisha wanamuziki wa Kanda ya Kaskazini wanapata
elimu ya kunufaika na kazi zao za sanaa kwani TAMUFO ni mkombozi wa
wasanii
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umetoa onyo kali kwa Redio Habari Maalumu
Kuhakikisha haisambazi nyimbo za wasanii bila kufuata utaratibu halali.
Onyo hilo
limetolewa na Rais wa TAMUFO Dk. Donald Kisanga katika mkutano
uliowakutanisha TAMUFO na vionozi wa redio hiyo pamoja na wadau wengine.
“Baada ya
kupokea malalamiko kutoka kwa Kwaya kongwe hapa nchini kuhusu kazi zao
kutumiwa na redio hilo bila faida tuliamua kufanya ziara ya kikazi
jijini Arusha kwa ajili yakuja kuyatafutia ufumbuzi malalamiko hayo na
kuongea na wahusika” alisema Kisanga.
Kisanga
alizitaja kwaya zilizotoa malalamiko kuwa ni Ulyankulu Mapigano na
Ulyankulu Barabara ya 13 zote za Tabora na Kwaya Kuu Habari Njema Kwaya
ya Uinjilist za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mjini kati zote za
Mkoani Arusha.
Alisema
TAMUFO baada ya kupokea malalamiko hayo iliweza kuwakutanisha Vikundi
hivyo vya kwaya Pamoja na redio hiyo na kumaliza mgogoro huo ambapo
walifikia muafaka kwa makubaliano kwa Kwaya husika iliitaka redio hiyo
iwalipe gharama za usumbufu.
Baada ya
Makubaliano hayo Dk. Kisanga aliwaonya Redio Habari Maalum kuacha mara
moja kuendelea kuuza kazi za Wanakwaya pasipo kuwa na mkataba.
Viongozi
wa TAMUFO bado wapo katika ziara ya kikazi mikoa ya Kanda ya Kaskazini
kukutana na wadau wa muziki wa injili ili kujua changamoto zao na
kuzitafutia ufumbuzi.
No comments :
Post a Comment