Wednesday, July 18, 2018

Mshindi wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 kuchachangia milioni mbili ujenzi wa kituo cha Polisi Mbagala,Temeke


 Katibu
Tawala wilaya ya Temeke Ndugu Hashimu Komba (kwa niaba ya MKuu wa
Wilaya),akimkabidhi Kombe la Tatu Mzuka kwa kijana mkazi wa
Mbagala,Abeid Amir aliyejinyakulia kitita cha shilingi Milioni
300,alipokwenda kutambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.Katika
mazungumzo yake na Uongozi wa Wilaya mshindi huyo ameahidi kuchangia
kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo
cha Polisi kinachojengwa Mbagala.
 Mshindi
wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 Abeid Amir akipokelewa kwa
shangwe,nderemo na vifijo  mara baada ya kuwasili nyumbani kwao
Mbagala-Kilungule,ambapo pia alipokelewa vyema na viongozi wa serikali
ya Mtaa kwa heshima kubwa.
 
Mshindi
wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018 Abeid Amir akipokelewa kwa
shangwe na Diwani wa Kata ya Kilungule Said Fella na akiwa sambamba na
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kata ya Zomboko Ndugu Hemed Said
Njiwa,mara alipowasili nyumbani kwao
Mbagala-Kilungule
Diwani
wa Kata ya Kilungule Said Fella akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kumpokea mshindi
huyo wa Milioni 300 za Supa Mzuka Cup 2018.

No comments :

Post a Comment