| Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga (Mb.) aliyesimama katikakti akiwa katika picha ya pamoja na
Waheshimiwa Mabalozi waliomaliza muda wao wa uwakilishi nchiniTanzania.
Mabalozi hao, wakwanza kutoka kushoto ni Balozi wa Norway, Mhe.
Hanne-Marie Kaarstad, Balozi wa Malawi, Mhe. Hawa Olga Ndilowe, Balozi
wa Sweden, Mhe. Katarina Rangnitt na Balozi wa Canada, Mhe. Ian Myles.
Mhe. Dkt. Mahiga aliandaa hafla ya kuwaaga Mabalozi hao iliyofanyika
jijini Dar Es Salaam tarehe 17 July 2018. Katika hafla hiyo, Dkt. Mahiga
aliwashukuru Mababalozi hao kwa niaba ya Serikali zao kwa mchango
mkubwa wanaotoa kuboresha sekta mbali mbali hapa nchni zikiwemo za
Elimu, Afya, Biashara, Kilimo pamoja na Miundombinu. Aidha, Mabalozi pia
walipata nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa Wizara pamoja na
watumishi wake kwa ujumla kwa kuwapa ushirikiano wa kutosha
uliowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hapa nchini. |
No comments :
Post a Comment