![]() |
WAZIRI
Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akinywa maji katika moja
ya Kisima ya miradi ya maji ya Kimbiji na Mpera wakati akikagua mradi
huo Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian
Masasi.
|
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa ametembelea mradi wa
uchimbaji wa visima virefu vya Kimbijii na Mpera wenye thamani ya
Bilioni 19.6 vitakavyosaidia kupatikana kwa lita za maji Milioni 260
kwa siku.
Mradi
huo wa visima vya maji uliochini ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar
es Salaam (DAWASA) una lengo la kuongeza wingi wa maji katika maeneo
mbalimbali ya Jijini Dar es Salaam na kufikia lita Milioni 720 kwa siku
kufikia mwaka 2032.
Prof
Mbarawa akiwa ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA Dkt Suphian
Masasi ameweza kukagua visima hivyo na kuwataka wakandarasi wa mradi huo
kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
Akizungumza
wakati wa kukagua visina hivyo, Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo
utawasaidia wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwa utasaidia upatikanaji wa
maji safi na salama na yatakayotosheleza kwa matumizi yao.
"
Mradi huu wa Kimbiji na Mpera utakaotoa Lita Milioni 260 kwa siku
utasaidia sana wananchi wa Dar es Salaam, ukichukulia Mradi wa Ruvu Juu
na Ruvu chini unatoa lita Milioni 502 kwa siku kwa ujumla wake utaleta
chachu ksa wananchi kupata maji kwa uhakika,"amesema Prof Mbarawa.
Amesema
kuwa, kukamilika kwa visima hivi kutaimarisha upatikanaji wa maji
katika maeneo ambayo hayakuwa na huduma nzuri ya majisafi na yale yasiyo
na mtandao rasmi.
Prof
Mbarawa akitoa maagizo mbele ya Mkurugenzi Wa DAWASA, ameitaka kampuni
ya Serengeti ya nchini Tanzania na Mkandarasi kutoka kampuni ya NSPT ya
nchini Iran kuhakikisha mradi huu unaenda na muda ulipangwa kwakuwa
tayari umesuasua kwa mrefu haujamalizika.
"
Kampuni yenu naipa wiki moja kwanza wawasilishe malipo ya bima kwa
wafanyakazi, vifaa pamoja visima vyenyewe ambapo gharama yake haizidi
hata Bilioni 4 na mkishafanya hivyo mniletee nione,"
Kwa
upande wa DAWASA, Kaimu Mkurugenzi Dkt Suphian Masasi amesema kuwa
wanategemea mradi huu uende kwa haraka zaidi ili wananchi wapate maji
ambapo wameona kuna baadhi ya maeneo wataamua kuyafanya wao kama Mamlaka
husika kama ununuaji wa vifaa, kuwalipa baadhi ya watendaji moja kwa
moja ili kuweza kurahisha umalizikaji wa kazi ili watu wapate maji.
"Sisi
tunafuata maagizo ya Waziri kwahiyo kinachofuata ni utendaji tu na kuna
maeneo tutawekea tija ikiwemo kuwalipa watendaji yawekezna ipo
changamoto ya ulipaji kwa wakati pia hata ununuaji wa vifaa tutafanya
hivyo pale inapohitajika na kisha baadae tutawakata katika malipo
yao,"amesema Dkt Masasi.
Naye
Msimamizi wa miradi ya Maji kutoka kampuni ya Dkt Charles Kaaya amesema
kuwa katika utafiti wao wa visima 19 ambavyo tayari vimekamilika
wanaimani upatikanaji wa maji utakuwa ni ule ambao umekadiriwa wa lita
Milioni 260 kwa siku.
Tayari
visima 19 kati ya 20 vya mradi wa Kimbini na Mpera vimekamilika na vina
kina kati ya mita 435 hafi 625 huku baadhi vikiwa na uwezo wa kuzalisha
lita 100,000 hadi 450,000 kwa saa na mradi huu umetekelezwa na serikali
ya Tanzania ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi wake wa Dar es
Salaam.
Maeneo
yatakayonufaika kwa mradio huo ni Kigamboni, Chanika, Chamazi, Pugu,
Kibada, Kisarawe 2, Kongowe, Gongo la Mboto, Segerea, Charambe, Buyuni,
Mbagala, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Tazara, Ukonga, eneo la viwanda la
Barabara ya Nyerere, Mji wa Mkuranga mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji
vyake vikiwemo Kisemvule na Kibamba.
WAZIRI
Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo
kutoka kwa Msimamizi wa miradi ya maji wa kampuni ya EGIS, Dk. Charles
Kaaya, kuhusu kupima urefu wa kisima kirefu katika mradi wa maji wa
visima virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasi.

WAZIRI
Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiwa pamoja Kaimu
Mkurugenzi wa DAWASA, Dk. Suphian Masasikatika mradi wa maji wa visima
virefu vya Kimbiji, wakati akikagua mradi huo Dar es Salaam
utakaofanikisha upatikanaji wa lita Milioni 260 kwa siku.




No comments :
Post a Comment