Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Miundombinu Mhe. Moshi Selemani Kakoso (wa tatu kulia) akishirikiana na
Naibu Waziri wa uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa
nne kulia) kukata utepe kuzindua mnara wakati wa wa ziara ya Kamati hiyo
ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Kumbulu
kilichopo wilayani Gairo, Morogoro. Wa tatu kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu-Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete na wa nne kushoto ni Mkuu wa
Wilaya hiyo Mhe. Sirieli Mchembe
Naibu Waziri wa uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akishuhudia
upatikanaji wa mawasiliano kwenye simu wakati wa ziara ya Kamati ya
Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji
cha Balama kilichopo wilayani Gairo mkoani Morogoro. Wa kwanza kulia ni
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Sirieli Mchembe na wengine ni wajumbe wa
kamati hiyo
Naibu Waziri wa uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiongea na wananchi wa kijiji
cha Balama kilichopo wilayani Gairo, Morogoro kuhusu jitihada za
Serikali za kujenga miundombinu ya mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati
ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye
kijiji hicho. Wa kwanza kulia ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Dua W.
Nkurua na wa kwanza kushoto mwenye miwani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Albert Richard
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Peter Ulanga akifafanua jambo kwa wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati wa ziara yao ya kukagua
upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Kumbulu kilichopo wilayani
Gairo mkoani Morogoro. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.
Moshi Selemani Kakoso na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipiga na
kucheza ngoma kabla ya uzinduzi wa mnara wa mawasiliano kwenye kijiji
cha Kumbulu kilichopo wilayani Gairo mkoani Morogoro wakati wa ziara ya
wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) ya kukagua
upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji hicho
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kushoto) akiungana na
wananchi kufurahia upatikanaji wa mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati
ya
Bunge ya Miundombinu ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye
kijiji cha Balama kilichopo wilayani Gairo, Morogoro. Wa pili kushoto ni
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Sirieli Mchembe na wa pili kulia ni mjumbe wa
Kamati hiyo Mhe. Bhagwanji Meisuria
…………………
Mkuu wa Wilaya ya Gairo iliyopo
Mkoani Morogoro Mhe. Sirieli Mchembe amesema kuwa upatikanaji wa huduma
za mawasiliano kwenye Wilaya hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kuinua
uchumi wa wananchi wake
Mhe. Mchembe ameyasema hayo wakati
wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea wilayani humo
kwa ajili ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwa wote kwenye maeneo
yasiyo na mvuto wa kibiashara kwa makampuni ya simu, maeneo yaliyopo
mipakani na yenye changamoto ya kijiografia kwa uwepo wa milima na
mabonde kama ilivyo katika wilaya hiyo.
Ameongeza kuwa wananchi wake
katika vijiji mbali mbali wanapata huduma za mawasiliano ikilinganisha
na hali ilivyokuwa hapo awali. Amefafanua kuwa mawasiliano yamefungua
fursa za kiuchumi kwa wananchi wake ambapo sasa wanaweza kuwasiliana na
kufahamu bei ya mazao katika masoko mbali mbali nchini kwa kuwa wilaya
hiyo inazalisha mazao ya biashara ya aina mbali mbali, kupata huduma za
ulinzi na usalama kwa haraka na kwa wakati, kurahisisha utoaji wa
taarifa zinazohusu afya za wananchi na upatikanaji wa huduma za matibabu
na kuwawezesha wanafunzi na waaalimu kujifunza na kufundishia. Mhe.
Mchembe ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada za kuhakikisha
kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano ambapo zimefungua fursa
mbali mbali.
Akiongoza ziara hiyo, Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Selemani Kakoso ameipongeza
Serikali kwa kujenga miundombinu ya mawasiliano kwa wananchi waishio
wilayani Gairo kwa kuzingatia changamoto ya kijiografia ya eneo hilo
ambapo sasa wanachi wanaweza kuwasiliana.
Kakoso amezitaka kampuni za simu
kuzipatia Serikali za vijiji mapato yanayotokana na uwepo wa minara ya
mawasiiano kwenye vijiji hivyo sehemu mbali mbali nchini ili mapato hayo
yawawezeshe wananchi kunufaika nayo kwa kuwekeza kwenye masuala mbali
mbali yanayogusa wananchi kama vile elimu na afya. Pia, amewataka
kampuni za simu za mkononi kuweka minara yenye nguvu ya kutosha ili
wananchi wapate mawasiliano wakati wote wa majira ya mwaka mzima na
nyakati za usiku na mchana.
Mhe. Kakoso ametoa rai kwa
wananchi kutunza minara kwa kuwa ni mali yao ambapo hapo awali walikosa
huduma hiyo na baadhi yao kupoteza uhai. Amesema kuwa, “tumieni nafasi
hii kuwekeza kwenye kilimo ili kutafuta masoko kwa kuwa Serikali
imetengeeza miundombinu ya mawasiliano na baraara kwa ajili yenu”.
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kwa kushirikiana na Mhe. Kakoso
na wajume wa Kamati wamezindua mnara wa mawasiliano uliopo kwenye kijiji
cha Kumbulu kilichopo wilaya ya Gairo mkoani Morogoro ambao umepewa
ruzuku na Serikali kupitia UCSAF ya kujenga mnara huo. Pia, uzinduzi huo
umeshuhudiwa na Mhe. Nchembe, viongozi mbali mbali wa Serikali wa
Wilaya hiyo na kamati ya ulinzi na usalama na wananchi waishio humo.
Pia, ameilekeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuanza kufuatilia
gharama za mawasiliano kwa kuwa wananchi wanaibiwa kwa kupiga simu
tofauti na muda wa maongezi walionunua kwa kuwa kuna baadhi ya kampuni
za simu wanafanya ulaghai kwa wananchi.
Pia, ameuelekeza Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ilete kompyuta tatu na vifaa vyake kwa kila
shule kwenye shule tatu za Kata ya Chanjale iliyopo wilayani Gario
mkoani Morogoro ili kuwawezesha wanafunzi na waalimu kusoma na
kufundishia kuendana na hali ya jiografia ya eneo hilo na ukuaji wa
Teknolojia ya Habari a Mawasiliano duniani. Mhandisi Nditiye amewaeleza
wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Magufuli iko tayari kuwahudumia wananchi na itaendelea
kuwahudumia
Mtendaji Mkuu wa UCSAF Mhandisi
Peter Ulanga amesema kuwa tayari UCSAF imefikisha mawasiliano kwenye
kata 530 sehemu mbali mbali nchini ambapo Serikali imezipatia ruzuku
kampuni hizo kujenga minara ya mawasiliano kwenye maeneo yasiyo na mvuto
wa kibiashara na yenye cangamoto za kijiografia kama ilivyo kwenye
Wilaya ya Gairo ambapo baadhi ya maeneo yana milima na mabonde hivyo
upatikanaji wa mawasiliano hapo awali ulikuwa ni changamoto.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
mnara huo, Meneja wa Kanda wa kampuni ya TIGO Bwana Joseph Mutalemwa
ameishukuru Serikali kwa kuwapatia ruzuku ya kujenga minara ya
mawasiliano ili kuweza kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi kwa
sababu wao wenyewe wasingeweza kujenga minara hiyo. Pia, ameongeza kuwa
wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali kufikisha mawasiliano kwa
wananchi kwenye sehemu mbali mbali nchini. Aidha, amefafanua kuwa uwepo
wa mawasiliano kwenye maeneo hayo unatoa ajira kwa wananchi.
No comments :
Post a Comment