Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wadau wa sekta ya maji
(hawapo pichani) wakati wa kongamano la kujadili fursa zilizopo na
changamoto zinazoikabili sekta binafsi nchini katika kuchangia maendeleo
ya sekta ya maji nchini.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wadau wa sekta ya maji wakati
wa kongamano la kujadili fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili
sekta binafsi nchini katika kuchangia maendeleo ya sekta ya maji nchini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wadau wa
sekta ya maji wakati wa kongamano la kujadili fursa zilizopo na
changamoto zinazoikabili sekta binafsi nchini katika kuchangia maendeleo
ya sekta ya maji nchini.
Baadhi ya wadau wa sekta ya maji
wakiwa katika kongamano la kujadili fursa zilizopo na changamoto
zinazoikabili sekta binafsi nchini katika kuchangia maendeleo ya sekta
ya maji nchini.
Mwakilishi toka sekta binafsi
nchini (TPSF) Louis Akaro akizungumza na wadau wa sekta ya maji wakati
wa kongamano la kujadili fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili
sekta binafsi nchini katika kuchangia maendeleo ya sekta ya maji nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Viwanda toka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Aristide Mbwasi
akizungumza na wadau wa sekta ya maji wakati wa kongamano la kujadili
fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili sekta binafsi nchini katika
kuchangia maendeleo ya sekta ya maji nchini.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
sekretarieti ya maandalizi ya kongamano la kujadili fursa zilizopo na
changamoto zinazoikabili sekta binafsi nchini katika kuchangia maendeleo
ya sekta ya maji nchini.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa (wa pili toka kulia) akipata maelekezo toka kwa
Afisa Mauzo wa kampuni ya Pipe Industries Ltd. Ezra Chiwelesa wakati wa
kongamano la kujadili fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili sekta
binafsi nchini katika kuchangia maendeleo ya sekta ya maji nchini,
Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Piyush Nath na wapili toka kushoyo
ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Prof. Makame Mbarawa akipata maelekezo ya vifaa vya maji toka kwa Afisa
Mauzo wa kampuni ya Plasco Ltd. Mhandisi Elisaria Aminiel wakati wa
kongamano la kujadili fursa zilizopo na changamoto zinazoikabili sekta
binafsi nchini katika kuchangia maendeleo ya sekta ya maji nchini.
Picha na MAELEZO
…………..
Kaulimbiu- “Kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi katika Kuendeleza Sekta ya Maji Nchini.” (19 – 20/07/2018)
Moto – Maji ni Uchumi
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
katika kutekeleza Program yake ya Pili (Water sector Development Program
II) – WSDP II) imeandaa Kongamano la siku mbili katika Ukumbi wa JNICC,
Dar es Salaam ambapo imewakutanisha wadau wa sekta ya Maji.
Walioshirikishwa ni watendaji
wakuu wa Idara za serikali sekta ya maji na Viwanda, Wakuu wa Mashirika
na Taasisi za Umma (MDAs; Washiriki wa Maendeleo (Development Partners) ,
Wakandarasi, Wawekezaji katika sekta ya Maji, mfano Water Aid, PIPE,
Kiboko Plastics, Kamal Steels; Wakandarasi; Washauri ; Sekta Binafsi
(TPSF).
Meza Kuu Mgeni rasmi alikuwa
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa, alifuatana na
Naibu Waziri wake na Katibu Mkuu na Naibu katibu Mkuu wake; Naibu
W#aziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Stela Manyaya (MB),ambaye
naye pia alifuatana Katibu Mkuu na naibu wake kutoka Wizara yake ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Pia meza kuu ilikuwa na Mwakilishi
wa Shirika la Kimataifa la Miradi la Uingereza (DFDI) wakati chombo cha
wawakilishi wa sekta binafsi (TPSF) kiliwakilishwa.
Mh. Profesa Mbalawa amefungua
Kongamano kwa kutoa onyo kwa watendaji wa sekta ya Maji kwa kuwataka
watende kazi kwa akilini na uweledi na waache vitendo vya ubabaishaji.
Ametoa mfano kuwa kwa muda mfupi aliokaa Wizara hiyo ya Maji na
Uwekezaji amegundua miradi mingi kutekelezwa kwa uzembe, kutoa tenda kwa
makandarasi wasiokuwa na uwezo, wasimamizi kutosimamia vizuri miradi na
waandalizi wa miradi kuandaa ovyo miradi kutokana labda kuwa na uwezo
mdogo ama kulipua kazi.
amesema serikali inaamini
itakamilisha lengo lake la kufikia malengo ya melinia (2015 – 2020) kama
ilivyojizatiti na hivyo ni wajibu wa kila mtendaji wa sekta ya maji
kujipanga kwa nafasi yake kwa kuhakikisha anatimiza wajibu wake na
kuonya kuwa yule asiyeweza ni bora awapishwe wanaoweza ili pasiwepo na
kukwama kwa yale yaliyokusudiwa kutekelezwa.
Waziri Prof Mbawara amesema katika
Programu ya Kwanza (WSDP I) serikali ililenga kuacha mwelekeo wake wa
kuendesha miradi ya maji yenyewe na kushirikisha sekta binafsi. Programi
hiyo iliyoanza Julai 2007 – 2016) ilishirikisha sekta binafsi katika
kubuni kupanga na kujenga miundombinu ya maji lakini tadhmini yake emona
mafanikia madogo.
Programu ya kwanza iliyotumia
trilioni 3.076 iligundua mapungufu ya baadhi ya miradi kutokamilishwa;
kujengwa lakini kutokuwa katika viwango vya ufanisi; ama kuchukua muda
mrefu mno kukamilika.
Lengo kuu sasa katika Programu hii
ya pili ni kuona kuwa kuna kasi ya utekelezaji wa miradi na kuona kuwa
inatekelezeka kwa ufanisi unaokusudiwa, kadhalika kushirikisha sekta
binafsi katika kubuni, kupanga kujenga (miundombinu) na kutoa huduma ya
maji.
Matarajio yake ni kuwa Kongamano
hili la siku mbili ni kuja na mapendekezo ya kuleta nguvu moja baina ya
serikali na sekta binafsi katika kufanikisha malengo ya serikali katika
sekta ya maji.
Kwa upande wake Naibu waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya, amehimiza wawekezaji,
wafanyabiashar na wananchi kwa jumla kusoma andiko la serikali
linalolenga kuleta mageuzi makuwa katika sekta ya biashara na uwekezaji,
ambapo serikali kwa kushirikisha sekta binafsi imepitia sera, sheria,
mifumo na miongozo inayosimamia sekta ya biashara, viwanda na uwekezaji
na kubainaisha kero na changamoto ambazo zinakusudiwa kuondolewa.
Majadiliano yameendelea mchana wa
leo na washiriki wataendelea na kesho kujadili jinsi ya sekta binafsi
kuboresha mahusiano na kubuni mawazo mapya katika kufanikisha sekta
binafsi kutoa huduma ya maji ambapo kwa sasa huduma hizo zinatolewa na
serikali kupitia chombo chake cha mamlaka za huduma za maji mijini.
No comments :
Post a Comment